Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawa: Watapata tabu sana

Dar es Salaam.BEKI wa Simba, Paschal Wawa, amefurahia kombinesheni yake na Erasto Nyoni na kutamka kuwa itawasumbua washambuliaji wa timu pinzania kupenya ngome yao.

Wawa alianza kwa kiwango cha kusuasua kwenye mechi za kirafiki lakini ameonekana kuanza kuimarika kadri anavyopewa mechi nyingi za kucheza hasa anapopangwa na Nyoni ambaye waliwahi kucheza wote Azam.

“Mimi na Nyoni tunafahamiana muda mrefu kwahiyo tunapocheza tunakuwa na lengo moja tu la kuhakikisha tunaisaidia timu yetu iweze kufanya vizuri, nashukuru Mungu tumetoka na ushindi,” alisema.

Akizungumzia ugumu wa washambuliaji wa Ligi Kuu, alisema ni hali ya kawaida kwa mshambuliaji yoyote kutaka kufunga, lakini umakini wa mabeki ndio unaweza ukafupisha safari yao.

“Najua washambuliaji wanataka kupata magoli kila mara ndio maana na mimi napambana vilivyo kuhakikisha kwamba nakuwa fiti kupambana nao, kazi yao ni kufunga na sisi kuzuia,” alisema.