Yanga wasubiri Manji kutengua uamuzi
Muktasari:
Uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika umeeleza kwamba kuchelewa kujibu barua ya kuombwa atengue maamuzi ya kujiuzulu wadhifa wake huenda kigogo huyo akawa na majukumu mengi yamembana.
Mkutano wa Yanga uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam mwezi uliopita, miongoni mwa maazimio yake ilikuwa ni wanachama hao kuazimia Yusup Manji kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti.
Uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika umeeleza kwamba kuchelewa kujibu barua ya kuombwa atengue maamuzi ya kujiuzulu wadhifa wake huenda kigogo huyo akawa na majukumu mengi yamembana.
Nyika ameeleza kuwa bado Manji kweli hajajibu barua yao na ikumbukwe katika Mkutano Mkuu wa wanachama wa klabu hiyo waliazimia kupinga kujiuzulu kwake na kupendekeza aendelee kuwa mwenyekiti wao.
Mwenyekiti huyo amefafanua kwa kusema yawezekana labda akawa ametingwa na majukumu yake binafsi kikazi hivyo mpaka sasa
Nyika alisemawamempa muda mpaka pale atakapopata nafasi ya kuwajibu kwa maana hivi sasa bado hakuna chochote ambacho kimewafikia kutoka kwake tangu wamtumie barua hiyo.
Kupitia Kamati ya kuipigania Yanga wakati wa Mpito, Nyika amesema inaendelea kufanya kazi ya kusaka fedha kwa ajili ya kuisaidia Yanga ili iweze kufanya usajili na kuiwezesha klabu kuhusiana na ulipaji wa mishahara ya wachezaji.
Nyika ameielezea kamati hiyo kuwa si kwamba inatoa fedha bali inafanya mipango ya kutafuta watu watakaotoa fedha ili klabu ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwemo usajili na mengine.