Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chirwa agomea pesa Yanga

Muktasari:

  • Chirwa kukataa kupokea pesa aliyokuwa anampa kama zawadi ambayo ililikuwa ni noti ya Sh10,000.

STRAIKA wa Yanga, Obrey Chirwa, ni mtata usiambiwe. Achana na  visa vyake kadhaa alivyofanya kipindi cha nyuma, staa huyo sasa  amekwenda mbali na kugomea minoti ya watu wa Yanga.

Chirwa ambaye amewahi kugoma mara mbili ndani ya Yanga akishinikizwa  kulipwa fedha zake za usajili pamoja na mishahara yake, awamu hii  amezua kubwa zaidi baada kugomea pesa.

Baada ya mashabiki wa Yanga kumzodoa staa huyo kwenye mitandao ya  kijamii baada ya kukosa penalti iliyowaondosha kwenye Kombe la Mapinduzi, wikiendi iliyopita aliibuka shujaa kwa kuisaidia timu yake  kuifunga Azam FC mabao 2-1, lakini hapo hapo akalizua la kugomea pesa.

Si unajua ni kawaida kwa wachezaji wa timu mbalimbali hasa wa  Simba na Yanga kila mechi inapomalizika mashabiki huwa wanakwenda  kuwapongeza kwa kuwapa pesa na zawadi mbali mbalimbali?

Lakini, sasa shabiki mmoja pale Chamazi ilimbidi awe mpole baada ya Chirwa kukataa kupokea pesa aliyokuwa anampa kama zawadi ambayo ililikuwa ni noti ya Sh10,000.

Shabiki huyo alipoona mechi ya Yanga na Azam imemalizika na wachezaji wanatoka ndani ya uwanja kwenda vyumbani, alimkimbilia Chirwa na kumpa pesa hiyo, lakini Chirwa alimnyooshea mkono kumuonyesha ishara ya kukataa.

Hata hivyo shabiki huyo kindakindaki wa Yanga alipoona Chirwa amekataa alimkimbilia Gadiel Michael na kumpa.

ROSTAND FRESH

Wakati huo huo, kipa wa Yanga, Youthe Rostand, amesema mashabiki waliokuwa wakibeza uwezo wake watulize mzuka kwani amepanga kufanya makubwa na timu hiyo hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

Rostand alisema anatambua kwamba mashabiki walikuwa wameanza kukosa  imani naye hasa katika upande wa penalti, hivyo alikuwa akijifua ili kuwa fiti na kumaliza tatizo hilo. Kipa huyo aliibeba Yanga kwenye mikwaju ya penalti dhidi ya Ihefu FC katika Kombe la FA ambapo sasa wametinga hatua ya 16 Bora.

“Siku zote likitokea jambo baya huwezi kulijibu kwa maneno, inabidi uwajibu kwa kusahihisha lile tatizo ambalo lilizua maneno. Nashukuru Mungu zoezi langu limeanza kukamilika kidogo kidogo, nitakuwa nafanyia kazi zaidi,” alisema.

“Tunajua kwamba mashabiki wanataka matokeo mazuri muda wote, tutahakikisha tunapambana ili tuweze kusonga mbele katika mashindano ya kimataifa. Mimi, Kabwili (Ramadhani) na Kakolanya (Beno) wote tupo vizuri katika kulinda lango, hivyo hatutowaangusha, hata wachezaji wengine nao wanafanya vizuri kwenye nafasi zao, tutatumia mashindano haya kujitangaza,”  alisema.