Zahera amzuia Ajibu Msimbazi
Muktasari:
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewaambia mabosi wake kwamba bado anataka kubakia na mshambuliaji wake zaidi Ibrahim Ajib.
Zahera amesema Yanga haitakiwi kumpoteza Ajib mwisho wa msimu wakati mkataba wake ukifikia ukiongoni.
Amesema mabosi wake wanatakiwa kuanza mazungumzo haraka kumbakisha mshambuliaji huyo na hatafurahi kusikia ameondoka na kwenda klabu nyingine na kwamba bado anahitaji huduma ya Ajib Zaidi katika timu hiyo.
IBRAHIM Ajibu 'Akadabra' amehusika na mabao sita kati ya 9 ya Yanga msimu huu, huku mashabiki wa Msimbazi wakimmezea mate kutokana na kuonekana kurejea upya, lakini jambo hilo limemshtua Kocha Mwinyi Zahera na kuamua kutoa maagizo haraka.
Zahera anafahamu kuwa, Ajibu mkataba wake unaelekea ukingoni na kwa kutambua kuwa jamaa ni bonge la mchezaji, amewaagiza mabosi wa Jangwani kufanya kila njia ili wampe mkataba mpya kabla aliokuwa nao haujaisha kabisa.
Akizungumza na Mwanaspoti, Zahera alisema licha ya Ajibu kutofanya vizuri kama alivyotarajia katika pambano la watani, haipotezi maana kuwa mshambuliaji huyo ni moja kati ya mtu hatari aliyenaye katika kikosi chake.
Zahera alisema bado anamhitaji sana Ajibu katika kikosi chake na kwamba anatambua mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu ana anataka abaki hapo.
Mkongomani huyo alisema tayari ameshawaambia mabosi wake kwamba wanatakiwa kuanza mapema mazungumzo ya kumuongeza mkataba mshambuliaji huyo kutokana na kuna vitu anavitaka kutoka kwake kuipa Yanga makali.
Alisema hazitakuwa taarifa nzuri kwake kusikia Ajibu amechukuliwa na timu pinzani ambapo kuhusu mapungufu yake ataendelea kuyafanyia kazi taratibu.
"Nimewaambia viongozi kwamba mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu wanatakiwa wasisubiri mpaka umalizike wanatakiwa kumuongezea mwingine. Niseme wazi sitafurahi kusikia Ajibu amechukuliwa na timu nyingine kuna mambo nataka kuyabadilisha hapa na Ajib ni mmoja ya watu ninaowahitaji katika timu yangu," alisema.
AMPA KAZI MWANDILA
Katika hatua nyingine, Kocha Zahera amempa majukumu Msaidizi wake, Noel Mwandila kuiongoza timu hiyo kwa mechi zilizopo mbele yao wakati yeye akienda kutekeleza majukumu ya timu ya taifa ya nchini kwaom DR Congo.
"Siwezi kukwambia programu gani nimemuachia, ila kwa vile naenda nyumbani nimempa kazi Mwandila ahakikishe tunazoa alama tatu mbele ya Mbao FC," alisema Zahera.
"Namuamini na naamini atayafanyia kazi kikubwa ninachotamani zaidi nisikute kimebadilika ni kupoteza pointi tatu hasa katika michezo ya nyumbani ni mipango ambayo tuliipanga kabla ya ligi kuanza baada ya kutazama ratiba tulikubaliana kuhakikisha tunavuna pointi zote nyumbani," alisema.
Zahera alisema majukumu aliyonayo katika taifa lake ni muhimu sana na ndio maana kaamua kuondoka mapema kuhakikisha anaisimamia timu yake hiyo ya Taifa kupata matokeo mazuri na kupata nafasi ya kufuzu kushiriki mashindano ya Afcon.
Yanga imeshinda michezo minne kati ya mitano iliyocheza, ikiambulia sare dhidi ya Simba, huku ikizifunga Mtibwa Sugar (2-1), Coastal Union (1-0), Stand United (4-3) na Singida United 2-0 na kufikisha alama 13 ikiwa nafasi ya nne.
"Ajib ndiyo hakufanya vizuri sana kama nilivyotarajia katika mchezo na Simba lakini haimaniishi kwamba hafai ni mshambuliaji ambaye namuhitaji sana hapa Yanga,"alisema Zahera.
"Nimewaambia viongozi kwamba mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu wanatakiwa wasisubiri mpaka umalizike wanatakiwa kumuongezea mwingine.
"Sitafurahi kusikia Ajib amechukuliwa na timu nyingine kuna mambo nataka kuyabadilisha hapa na Ajib ni mmoja ya watu ninaowahitaji katika timu yangu."
***
finite
Summary
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewaambia mabosi wake kwamba bado anataka kubakia na mshambuliaji wake zaidi Ibrahim Ajib.
Zahera amesema Yanga haitakiwi kumpoteza Ajib mwisho wa msimu wakati mkataba wake ukifikia ukiongoni.
Amesema mabosi wake wanatakiwa kuanza mazungumzo haraka kumbakisha mshambuliaji huyo na hatafurahi kusikia ameondoka na kwenda klabu nyingine na kwamba bado anahitaji huduma ya Ajib Zaidi katika timu hiyo.