Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yazidi rekodi nyingine Simba

Muktasari:

Yanga haitashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, lakini bwana timu hiyo imeipiga bo Simba nje ndani, sambamba na kuziburuza klabu nyingine za Afrika Mashariki kwa ufanisi wake tangu mwaka 2000.

HAKUNA ubishi Yanga haitoshiriki michuano yoyote ya kimataifa kwa msimu ujao, yaani haitacheza  Ligi ya Mabingwa wala Kombe la Shirikisho Afrika, lakini asikuambie mtu mabingwa hao wa Kihistoria wameipiga bao watani zao, Simba nje ndani.
Yanga imewekea rekodi mbili ngumu ambazo watani wake Simba na timu nyingine nane kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki zitapaswa kufanya kazi ya ziada kuzivunja.
Klabu 10 za  Afrika Mashariki licha ya kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho msimu ujao, kirekodi zimeonekana kushindwa kufua dafu mbele ya Yanga ambayo haitoshiriki baada ya kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu na Kombe la FA msimu uliopita.
Rekodi ya kwanza ya Yanga ambayo klabu hizo za nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ikiwemo Simba, zinapaswa kuivunja ni ya kufuzu mara nyingi zaidi katika hatua ya makundi ama ya Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho.
Ukiondoa KCCA ya Uganda ambayo inaonekana ndio timu pekee Afrika Mashariki inayoweza kupindua rekodi ya Yanga ikiwa nayo imefuzu mara mbili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho au Ligi ya Mabingwa, kuanzia mwaka 2000 hadi sasa hakuna nyingine yoyote ya Ukanda huu iliyofanya hivyo.
Wakati Yanga ilifuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho 2016 kabla ya kufanya hivyo tena mwaka huu, KCCA yenyewe ilifuzu makundi ya Shirikisho Afrika 2017 kabla ya mwaka huu kufuzu hatua hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Rekodi nyingine ambayo Yanga inatamba nayo ni ya kushiriki kwenye mashindano ya klabu Barani Afrika mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine katika kipindi cha miaka 18, kinachoanzia mwaka 2000 hadi sasa. Katika kipindi hicho, Yanga imeshiriki mara 15.
Simba yenyewe imeshiriki mara 12 na hivyo ushiriki wake msimu ujao, utaifanya idaiwe na Yanga kushiriki mara moja nyingine ili waende sawa.
Ukiondoa Simba na KCCA, zitakazowakilisha ukanda huo wa Afrika Mashariki Le Messager Ngozi na Vital'O (Burundi), Vipers (Uganda), APR na Mukura (Rwanda), Mtibwa na Gor Mahia (Kenya)

Zahera abeba tuzo
Katrika hatua nyingine, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Septemba akifuata nyayo za Amri Said wa Mbao aliyebeba kwa Agosti, huku Eliud Ambokile wa Mbeya City akinyakua tuzo ya Mchezaji Bora kwa Septemba.
Tuzo hizo za Makocha ni za kwanza katika Ligi Kuu na zinatolewa na Kamati ya Tuzo za Wachezaji wa Ligi Kuu Bara. Ambokile amefuata nyayo za Meddie Kagere aliyebeba kwa Agosti akiwa kwa sasa ndiye kinara wa ufungaji akifunga mabao sita.