Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaapa ubingwa wa Ligi Kuu kutua Jangwani

Muktasari:

  • Kwa upande wa kiungo wa timu hiyo, Fei Toto anasema nguvu yao kwa sasa wanaihamishia kwenye ligi kuendeleza mapambano mpaka dakika ya mwisho kuona watavuna nini.

KAMA unadhani mastaa wa Yanga wamekata tamaa baada ya kuenguliwa nusu fainali za Kombe la FA, kwa kufungwa na Lipuli mabao 2-0 basi itakula kwako kwani wamekuja na kubwa kuliko.

Beki wa timu hiyo, Andrew Vicent 'Dante' amesema wao ni kama askari baada ya kudondosha tiketi ya kushiriki Shirikisho Afrika kwa sasa wanatabanana kwenye Ligi Kuu.

"Imetuuma sana na mashabiki wetu watuwie radhi kwani tulipambana ila bahati haikuwa kwetu, lakini nguvu yetu ya tone la mwisho tutaimalizia kwenye ligi kuu.

"Sisi hatutaki kuangalia Simba ina mechi nyingi mkono, tunacholinda tunaongoza ligi na tunatakiwa kushinda mechi zetu hayo mengine hayatuhusu"anasema.

Kwa upande wa kiungo wa timu hiyo, Fei Toto anasema nguvu yao kwa sasa wanaihamishia kwenye ligi kuendeleza mapambano mpaka dakika ya mwisho kuona watavuna nini.

"Malengo yetu ni ubingwa kikubwa sisi ni kushinda mechi zetu, hayo mengine yatajipanga yenyewe"anasema.