Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yajayo Kocha Mbelgiji wa Simba yanafurahisha!

Muktasari:

Sare mbili na kupoteza mechi moja kumemfanya kocha wa Simba, Patrick Aussems kupanga kufanya maamuzi magumu kwa nia ya kutaka kuifanya Simba ifike mbali katika mechi za Ligi Kuu na zile za kimataifa, huku nyota wake wakipata mzuka.

KIKOSI cha Simba, kesho Jumamosi kitavaana na African Lyon katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara, huku Kocha Mkuu wa timu hiyo akipewa mchongo wa kubadilisha mfumo wake, huku ikielezwa kuna uamuzi mgumu anatarajia kuufanya.

Uamuzi huo, Patrick Aussems una lengo la kutaka kuiona Simba ikifika wanakotaka hasa kutetea taji lao la Ligi Kuu na kufika mbali katika mechi za kimataifa, kama moja ya masharti aliyopewa wakati akisaini mkataba Msimbazi Julai mwaka huu.

Hatua ya kocha huyo kutaka kufanya uamuzi hayo magumu yanaweza kuwapa wakati mgumu baadhi ya nyota wa klabu hiyo na ishu imekuja huku aliyekuwa mmoja wa wasaili wa kocha huyo, Dk Mshindo Msolla kumshauri abadilishe mfumo ili anyookewe Simba.

Msola alisema Simba imevuna alama tano katika mechi nne zilizopita kwa sababu ya kutokuwa na mbinu mbadala timu yake inapolemewa, hasa kuamua kumuacha Msaidizi wake, Masoud Djuma katika mechi tatu zilizopita za ugenini na kuvuna alama nne tu..

Mechi ya mwisho ya ligi Aussems kuwa na msaidizi wake ni ya Yanga iliyoisha kwa suluhu na Kocha Msolla aliliambia Mwanaspoti, Aussems anapozidiwa hukosa njia mbadala ya kupata ushindi kutokana na mfumo wake anaoutumia wa 4-4-2.

Msolla alisema ili Simba watetee ubingwa ni lazima benchi la ufundi liwe na umoja na ushirikiano katika kushauriana mambo mbalimbali ya kiufundi ndipo watafikia malengo.

“Bahati nzuri nimeangalia mechi zote za Simba hata wakipata ushindi lakini wanapata ushindi wa mabao machache, Aussems ni kocha mzuri ila ana tatizo moja la kushindwa kuwa na mpango wa pili pale anapoona upatikanaji na mabao ni mdogo.

“Hata mechi ya Yanga walicheza mpira mzuri lakini hakuweza kupata ushindi na ni tatizo ndani ya Simba ambapo kocha mwingine anasoma mchezo na kubadilisha mfumo ila kwa Aussems hayupo hivyo hana mbinu mbadala, hilo litamsumbua sana anapaswa kubadilika, Simba wanahitaji matokeo mazuri kulingana na malengo yao,” alisema Dk Msolla.

MBELGIJI ASHTUKA

Licha ya Kocha Aussems kusisitiza kuwa, atakomaa na mfumo aliotumia dhidi ya Yanga, lakini inaelezwa katika mechi ya leo atafanya uamuzi mgumu katika kupangua kikosi chake ili kutengeneza njia ya kutetea taji lao msimu huu.

Habari za ndani zinasema kuwa, nyota waliokuwa hawaanzi kikosi wakiwamo Haruna Niyonzima na Juuko Murshid ameanza kuwapigia hesabu ya kuwatumia, hatua inayofanya baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza kupanguka.

“Kocha ameanza kuona ugumu wa Ligi na sasa anataka kufanya uamuzi mgumu ndani ya kikosi chake ili kuhakikisha malengo ya kutetea ubingwa na kufanya vyema katika mechi za kimataifa zinafanikiwa,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba aliyeomba kuhifadhiwa jina.

Mbelgiji huyo tangu atue Simba amekuwa akitumia wachezaji karibu wale wale wa kikosi cha kwanza ukiondoa Emmanuel Okwi, John Bocco na Meddie Kagere wanaobadilishana, lakini kwa kilichoelezwa mipango yake sasa ni kuona wengine wanapata nafasi zaidi.

TSHABALALA MZUKA

Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amefichua kuwa, suluhu dhidi ya Yanga imewapa mzuka nyota wa Simba na kuwataka mashabhiki wa klabu hiyo kutulia kwamba mambo mazuri yanaenda kutokea Msimbazi.

Tshabalala alisema sare mbili ikiwamo ile ya Ndanda FC na kipigo cha Mbao, kimewaamsha usingizi na sasa wanaenda kufanya kazi katika mechi zao zijazo.

“Nguvu na hali ya kukaa kieleni ipo juu, sare na kufungwa mchezo mmoja imetupa uchungu wa kuzing’oa timu zilizopo nafasi tatu za juu, hilo linawezekana na tumejipanga kuhakikisha mashabiki wetu wanaendelea kuwa na imani na timu yao.“Malengo yetu ni kuona tunafululiza kuchukua ubingwa, hilo linawezekana na ndio maana hatukatishwi tamaa na sare pamoja na mchezo tulioupoteza dhidi ya Mbao FC, tumechukulia kama moja ya changamoto ya kutufanya tuongeze umakini wa hali ya juu,” alisema.

DALALI AIBUKA

Wakati Tshabalala akisisitiza kupata nguvu mpya ya kupambana kukaa kileleni, aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo, Hassan Dalali ‘Mzee Dalali’ yeye alituma ujumbe wake kwa viongozi kujenga nguvu ya umoja kwa wanachama kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega mpaka mwisho wa msimu.

“Ukizizungumzia Simba na Yanga ujue wazi kwamba nyuma yake kuna nguvu kubwa ya mashabiki ambao ndio chachu ya timu hizo kuwa maarufu na kuonekana za tofauti kwenye ligi kuu Bara na kufanya mchezaji anayebahatika kuzitumikia kuandika historia ya aina yake iwe kwa kufanya vizuri ama ovyo zaidi.