Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sven apewa rungu la usajili

UONGOZI wa Simba haujaonyesha kuwa na papara badala yake wamempa nafasi ya kocha wao mpya Sven Vandenbroeck kuangalia wachezaji wake na kisha atoe kauli juu ya usajili.

Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa amesema kwamba licha ya dirisha la usajili kufunguliwa, hawawezi kusajili bila kuangalia matakwa ya benchi la ufundi.

"Tunamuacha kocha na benchi lake aangalie kikosi kilichopo ili ajue kama kuna mabadiliko ambayo yatahijika, hatuwezi kusajili mchezaji kama kocha hajasema," alisema.

Licha ya kwamba Senzo amempa rungu Sven kwenye usajili, bajeti ya Simba kwenye dirisha dogo kupitia mkutano mkuu ilitangazwa kuwa ni Sh 76 Milioni 76, ambapo imeelezwa kwamba wataangalia mapendekezo ya kocha kama yataendana na bajeti yao.

"Kila kitu kitaendana na matakwa ya kocha, tutajua mchezaji yupi  na atatoka wapi kulingana na bajeti tuliyonayo," alisem.