Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali: Uchaguzi Yanga SC lazima

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo alisema, lengo lao ni kuona uchaguzi huo unafanyika mapema Februari na wanaendelea kupambana kuhakikisha wanamaliza kesi zote zilizofunguliwa.

WAKATI kukiwa na sintofahamu ni lini Uchaguzi Mdogo wa Yanga utafanyika, tangu uliosimamishwa kutokana na kufunguliwa kwa kesi mahakamani, Serikali imesisitiza uchaguzi huo utafanyika ndani ya mwezi ujao kwani kuna kila dalili vikwazo kuondoka.

Uchaguzi huo umekuwa katika sintofahamu baada ya baadhi ya wanachama kufungua kesi Januari 11 kupinga mchakato wa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike Januari 13.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Ally Mchungahela alisisitiza mchakato wa uchaguzi huo utaendelea ndani ya siku saba tangu Januari 14, lakini umeshindikana kutokana na kesi inayoendelea mahakamani.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo alisema, lengo lao ni kuona uchaguzi huo unafanyika mapema Februari na wanaendelea kupambana kuhakikisha wanamaliza kesi zote zilizofunguliwa.

“Tulikuwa kwenye harakati za kumaliza kesi kadhaa zilizofunguliwa kuhusu uchaguzi, lakini asilimia kubwa tumezimaliza, imebaki kesi moja ya kupinga kadi za benki kutumika kwenye uchaguzi.

“Kesi hiyo ndio inatuchelewesha tunapambana kuifuta kwa kufuata hoja zote za waliofungua kesi hilo, kubwa ni kuhakikisha tunamaliza mapema kabla ya Februari, ili uchaguzi huo ufanyike ndani ya mwezi huo kama ilivyopangwa awali klabu hiyo kuziba nafasi zilizo wazi,” alisema.

Singo alisema hawapendi kuwa karibu sana na vyombo vya habari kuhusiana na suala hilo la uchaguzi kutokana na kuendeshwa kisheria zaidi na kuweka wazi mambo yatakapokuwa sawa watatolea ufafanuzi na kupanga tarehe ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo uliitishwa na Serikali kupitia TFF ili kuziba nafasi sita zilizoachwa wazi katika klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani za mwenyekiti iliyokuwa inashikiliwa na Yusuf Manji, makamu mwenyekiti iliyoachwa na Clement Sanga na wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo yenye mashabiki wengi na kongwe hapa nchini.