Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adeyum ninadeni kubwa Yanga ila muda utaongea

Muktasari:

Adeyum amejiunga na Yanga akitokea JKT Tanzania ni miongoi mwa nyota watakaoshuka uwanjani kesho kumenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi.

Dar es Salaam.Beki mpya wa Yanga, Adeyum Saleh amesema bado anadeni kubwa kwa Wanayanga ila muda utaongea zaidi.

Adeyum amecheza mechi tatu akiwa na Yanga dhidi ya Biashara United na Simba pamoja na mechi ya jana dhidi ya Jamhuri aliyofunga Yanga ikishinda 2-0 katika Kombe la Mapinduzi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Adeyum alisema haijawa rahisi kwake kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza hivyo atapambana muda wote lengo ni kuona namba yake haipotei kikosini.

"Najua kuna mashabiki wengi hawana imani na mimi ninachoweza kuwaambia ni kwamba muda utaongea nina michezo mingi ya kuchezo hivyo nitaendelea kupambana zaidi lengo ni kuona mchango wangu kwenye timu unaonekana hilo linawezekana," alisema.

"Mafanikio ninayoyapata sasa hayanivimbishi kichwa ndio kwanza yananipa nguvu za kuendelea kupambana zaidi naamini kama nitaendelea kuaminiwa zaidi naweza kuifanyia Yanga kitu kikubwa na mimi mwenyewqe kuendeleza kipaji changu kwa mafanikio," alisema Adeyum.