Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba: Heshima inakuja kwa kutwaa mataji yote Tanzania

Muktasari:

Nje na mechi ya KMC, Azam na Simba pia alisema anatamani kuona wanavuna pointi sita mkoani Mbeya dhidi ya Prisons na Mbeya City ambako mtu ukishinda unaona fahari kutokana na ugumu wake.

Simba wanataka kutwaa ubingwa wa mataji yote kwa kishindo kwa imani kwamba jambo hilo litaweka heshima kubwa kwao katika soka la Tanzania.
Nyota wa timu wanataka kushinda mechi zote ngumu kwa kuanzia hii ya Machi 8 dhidi ya Yanga.
Kiungo wa Wekundu wa Msimbazi, Jonas Mkude amesema anajua kwamba kabla ya kuwafikia Yanga, mbale yao kuna mechi mbili ya Namungo na Azam FC na kwamba zote hiz nyota wa Simba wamedhamiria kutoa vipigio vikali.
Anaamini kwamba wakishinda hizo zitawapa morali zaidi ya kupambana ili kufikia malengo yao.
“Ingawa kwa mchezaji hakuna mechi rahisi lakini kuna zile ambazo mashabiki wanakuwa na shaka, hizo ndizo tunazotamani kushinda kwa kishindo ili tukitetea ubingwa iwe kwa kishindo,” alisema mchezaji huyo aliyeko kwenye hatihati ya kufungiwa baada ya kupelekwa kamati ya nidhamu.
Aliongeza:  “Sio kazi rahisi lakini naamini kila mchezaji akituliza akili yake kila kitu kitafanyika kwa mafanikio ya hali ya juu.”
Nje na mechi ya KMC, Azam na Simba pia alisema anatamani kuona wanavuna pointi sita mkoani Mbeya dhidi ya Prisons na Mbeya City ambako mtu ukishinda unaona fahari kutokana na ugumu wake.