Mkude anataka heshima Bara

Muktasari:

Jonas Mkude ana mahesabu makali msimu huu anatamani kikosi chao kimalize ligi kikiwa na pointi 104 ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani wao.

KIUNGO Jonas Mkude amesema kiu yake na wachezaji wenzake wa Simba ni kuona wanamaliza msimu kwa heshima kwa kutetea taji lao la Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo.
Mchezaji huyo mwandimizi ndani ya Simba amesema pointi walizonazo na mechi zilizosalia kwao ni nafasi ya kupambana kuziongeza ili kuchukua taji mapema kabla ligi9 haijaisha na hiyo itakuwa heshima kwao.
"Ligi ni ngumu unapokuwa kileleni inakupa nguvu ya kuongeza juhudi zaidi ukijua kuna timu inayotamani kuwaondoa ndio maana ya kuwania taji la ligi kuu," alisema Mkude aliyeifungia mabao moja katika msimu huu na kuongeza; "Tunatamani kumaliza ligi kibabe, japo tunatambua kwamba si kazi rahisi kwani tunakwenda kucheza na timu zinazojikwamua kushuka daraja, hivyo zitakuwa mechi za kisasi."
Mkude amesema wanatamani kuandika rekodi ya kuchukua ubingwa mara tatu mfululizo ili kutimiza lengo lao na kuweka heshima mbele ya mashabiki wa Simba na wale wa soka la Tanzania kwa ujumla.