Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbelgiji sasa kawageukia Kagere, Okwi

Muktasari:

MASTRAIKA wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wamecheza kwa pamoja katika mechi tatu ambapo, hawajafunga bao lolote msimu huu, licha ya kuonekana kuwa miongoni mwa washambuliaji hatari nchini.
Kagere na Okwi wamecheza mechi dhidi ya Ndanda, Mbao na Yanga na kushindwa kufunga hata bao moja huku kila mmoja akiwa na rekodi matata kwenye Ligi Kuu Bara.

Kagere amefunga mabao manne dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City na Mwadui FC, lakini kwenye mechi zote hizo alicheza sambamba na John Bocco.

Okwi, raia wa Uganda alikuwa Mfungaji Bora msimu uliopita akifunga mabao 20, hajafunga bao lolote mpaka sasa ligi ikielekea mzunguko wa sita.

Lakini, Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa hajafurahishwa na matokeo hayo dhidi ya Yanga na sasa anajiandaa kufanya kitu ikiwemo kuwapa mbinu mpya mastraika wake ili kuongeza makali.

Pia, amesema kuwa kama mastraika wake wangekuwa makini kwenye mchezo huo, wangepasia nyavuni hata mabao matatu lakini, kukosa kwao umakini na utulivu kumechangia matokeo hayo.

“Ni kweli, wamecheza mechi tatu bila kufunga si jambo zuri kwa timu, nitabadili mbinu na kuwapa mpya ili kuongeza makali. Nataka kuwaongezea umakini na utulivu pindi wanapopata nafasi za kufunga ili kuleta matokeo mazuri.

“Kagere anakutana na changamoto kutokana na kasi yake ya kufunga, kila beki anatamani kumkaba na kumzuia asifunge, lakini Okwi anakosa utulivu na kutokujiamini ndio sababu hajafunga mpaka sasa, japo ni mzuri sana,” alisema Aussems.