Mashabiki wa Simba kuifuata Nkana kwa basi

Muktasari:

 

Simba inatarajiwa kucheza mchezo wake dhidi ya Nkana Red Devils nchini Zambia Jumamosi Desemba 15 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umesema kwamba mashabiki wa klabu ya Simba wanatarajia kuondoka kesho Alhamisi kwenda nchini Zambia ili kuipa sapoti timu yao inayocheza Jumamosi dhidi ya Nkana.

Mashabiki hao wa Simba wanatarajiwa kusafiri kwa basi la klabu ya Simba kupitia  Tunduma jijini Mbeya na wanatarajia kuwasili keshokutwa Ijumaa.

Tayari kikosi cha Simba imeshatangulia nchini Zambia ambapo, taarifa ya klabu ilieleza kwamba Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Francis Ndulane ndiye ameongozana na klabu hiyo.

Jumla ya wachezaji 20 benchi la ufundi sita, wakiongozwa na Kocha Mkuu, Patrick Assems pamoja na viongozi wengine watatu pia wamesafiri.

Simba ilifuzu kuendelea hayua inayofuata baada ya kuiondoa Mbabane Swallows kwa jumla ya mabao 8-1 jambo ambalo limefufua matumaini kwa timu hiyo kufika mbali zaidi kwenye mashindano haya.