Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manji apewa majina

Muktasari:

  • Hafidh kila Mwanayanga anatambua mchango wa Bossou katika misimu miwili aliyoitumikia timu yetu mimi ni kweli nina mawasiliano naye ya karibu na kila mara ananishawishi niongee na viongozi aweze kurudi.

ACHANA na shangwe la wachezaji wa Yanga baada ya kusikia Mwenyekiti wao, Yusuf Manji amerejea katika nafasi yake, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera ghafla tu amefunguka akisema taarifa hizo zilizomshtua kisha akasema, kama mkubwa amerudi basi ubingwa Yanga ni mali yao.

Pia, Zahera amesema mkakati wake wa kusajili mastaa watatu wa maana ndani ya kikosi chake, umepata mzuka kwani, anaamini mabosi wa Kamati ya Usajili ikiongozwa na Hussen Nyika, watamkabidhi majina hayo.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka kwao DR Congo Zahera amesema kurejea kwa Manji na kama mambo yatatulia baada ya kurudi kwake, basi Yanga haiwezi kupishana na ubingwa msimu huu.

Alisema kila walipokuwa wakikutana na wakati mgumu katika timu yao walikuwa wanakumbushana kumwombea Manji ili mambo yakae sawa na arejee ili arudi klabuni.

Kocha huyo alisema kurejea kwa Manji kisha Yanga ikafanya usajili aliokusudia kuufanya, hakuna namna timu yake unaweza kuukosa ubingwa msimu huu.

Amesisitiza kuwa akirejea ataliamsha kwa wachezaji wake kwa kuwataka kufanya kazi kwa nguvu zaidi kwani sasa matatizo yao yatashughulikiwa na uongozi na wao wanatakiwa kuchapa kazi.

“Nimeshtuka sana kusikia hizo taarifa, niliacha hata kula, nimefurahi sana hii ni habari njema kwangu na kwa Wanayanga wote wanaotaka mafanikio ya hii timu,” alisema Zahera.

“Hamjui kila wakati tulikuwa tunaambiana kwenye timu tuzidishe maombi tumwombee kiongozi wetu Manji arudi kila mchezaji na wasaidizi wangu wanajua nguvu ya bosi wetu.

“Nasema kama Manji amerudi halafu tukafanya usajili wa wachezaji watatu ambao, nataka kufanya kwenye dirisha dogo la Januari, sioni nani anaweza kuizuia Yanga isiwe bingwa.

“Tusubiri kuona lakini nikirudi wachezaji wangu wajiandae nataka tufanye kazi ya nguvu kuliko iliyofanyika nyuma ili tumrudishe kwa mafanikio kiongozi wetu, najua matatizo yao sasa yatashughulikiwa.

Wachezaji nao walipuka

Kule nchini Afrika Kusini walipo baadhi ya wachezaji wa Yanga katika kambi ya kikosi cha Taifa Stars ongeza na wale waliobaki nchini wamelipuka kwa furaha wakisema ‘bosi karudi’.

Kiungo Feisal Salum “Fei Toto alisema bado haamini licha ya kuona vipande vya video na picha juu ya kurejea kwa Manji.

“Mpaka sasa siamini hizo taarifa naona picha na video lakini nikimwona nitaamini zaidi hii ni habari njema kwetu,” alisema Fei Toto.

Naye beki Andrew Vincent “Dante alisema wamepokea kwa faraja taarifa hizo na sasa wanasubiri kutangaziwa rasmi na viongozi wao.

“Kusema kweli hakuna ambaye anaweza kusikia taarifa za Manji karudi alafu akanuna labda awe sio mtu anayetaka mafanikio ngoja tusubiri viongozi waje watutangazie kwanza,” alisema Dante

Bossou aomba kurudi

Aliyewahi kuwa beki wa kati wa Yanga, raia wa Togo Vincent Bossou ameomba kurejea ndani ya klabu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili, linalotarajiwa kufunguliwa Novemba 15.

Bossou aliichezea Yanga kwa mafanikio ndani ya misimu miwili mfululizo akijiunga na klabu hiyo Agosti 2015 na mara baada ya kumaliza mkataba wake alitimka nchini kutokana na Yanga kushindwa kufikia makubaliano na beki huyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mratibu wa Yanga, Saleh Hafidh alisema amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na nyota huyo akiomba kurejeshwa katika kikosini dirisha dogo la usajili ili aendelee kuisaidia timu hiyo ambayo haina msaidizi wa Yondani.

“Bossou amekuwa akiniomba sana arudi, sasa kwa kuwa kocha hayupo namsubiri arudi ili nimweleze kama atakubali kwa kuwa hata yeye alisema anahitaji kuongeza mchezaji katika nafasi hiyo,” alisema.

Kwa mujibu wa kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mwingi Zahera alikiri kutafuta beki wa kati ambaye ataongeza nguvu kikosini kwake dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Zahera, ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo, yupo nchini Congo wakijiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika mwakani (AFCON 2019) dhidi ya Congo Brazaville, mchezo utakaochezwa Novemba 18 alipotafutwa kwa ajili ya kuzungumzia hilo alisema kwa sasa yupo na majukumu ya timu yake ya taifa na kuombwa kutafuta baada ya kurejea nchini.

“Huku pia nipo kazini na nimeomba ruhusa kwa uongozi umenipa nafasi ya kuja kulitumikia taifa langu, ishu za Yanga kwa sasa siwezi kuzipa kipaumbele kwa sababu nipo nje ya majukumu naomba unitafute nikirejea nchini ili niweze kulizungumzia zaidi,” alisema.

Bossou aliyezaliwa Februari 7, mwaka 1986 mjini Kara, Togo, aliibukia klabu ya Maranatha FC ya kwao, kabla ya kusaini Etoile du Sahel ya Tunisia Januari 15, mwaka 2010 mkataba wa miaka miwili.

Nyota huyo alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo kilichojitoa AFCON ya mwaka 2010 Angola, baada ya basi la wachezaji kushambuliwa na majeshi ya waasi likiwa njiani kwenda kwenye fainali hizo.

Kunguruma Nov 24

Siku moja baada ya kutangazwa rasmi kurejea kwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Baraza la Wadhamini limeridhia kufanyika kwa mkutano mkuu wa dharura lakini habari zaidi zinasema Manji atahudhuria mkutano huo wa kwanza.

Kamati ya utendaji ya Yanga juzi iliagizwa na Baraza la Wadhamini kuandaa mkutano mkuu na haraka utekelezaji wake umefanyika.

Jana jioni Baraza la Wadhamini la Yanga limeridhia kufanyika kwa mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika Novemba 24, Mwanaspoti limefahamishwa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema Baraza la Wadhamini ambalo jana pia lilikutana kwa ukamilifu liliridhia mkutano huo. Taarifa zaidi zinasema katika mkutano huo, Manji amekubali kushiriki katika mkutano huo ambao kama atafika basi utakuwa mkutano wake wa kwanza tangu atangaze kujiuzulu.

“Tumefanya mkutano na kukubaliana ni bora tufanye mkutano wa dharura ili tuweze kuwekana sawa na mikutano kama hii ndiyo muhimu kutuunganisha,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji.

“Tunataraji pia mwenyekiti wetu Manji amethibitisha kuhudhuria, wanaotaka kusikia kauli yake basi wajiandae kumsikia siku hiyo.”