Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabingwa Burundi kuipima Yanga

Muktasari:

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Yanga kwa kucheza na timu ya kigeni ukiwa ni kipimo cha nne kwa timu hiyo tangu kianze kambi ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya.


YANGA inatarajiwa kucheza mchezo wa nne wa kirafiki kesho Jumamosi dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Noir.
Ikiwa kambini mkoani Morogoro, Yanga itacheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza kukutana na timu kutoka nje ya nchi.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema bado kocha wao msaidizi Noel Mwandila anahitaji mechi za kirafiki kukipima kikosi chake.
Saleh amesema mchezo huo utapigwa uwanja wa Highland Park ambao Yanga inautumia kwa mazoezi ambapo mabingwa hao tayari wametua Morogoro.
Hafidh amesema kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kucheza dhidi ya Mawenzi Market inayoshiriki ligi daraja la pili msimu ujao.
Noir tangu watua nchini wamecheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Namungo FC, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar walipoteza mbili na kutoa sare moja.
Timu hiyo awali imefungwa na Namungo kisha kupokea tena kipigo kutoka Kagera zote wakifungwa mabao 3-0 kila mmoja kisha kutoa suluhu ya bao 2-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.