Kichuya awaahidi mazito mashabiki Simba

Muktasari:

Kichuya ni mchezaji kipenzi cha mashabiki wa Simba Ndiye mchezaji pekee wa kikosi hicho ambaye ana bahati na wapinzani wao wakubwa Yanga.
Amewahi kuwafunga mara tatu. Akiwafunga Oktoba Mosi 2016 timu hizo  zilipotoka sare ya bao 1-1. Aliwafunga tena bao moja Februari 27,2017 Simba iliposhinda mabao 2-1 na kisha akawafunga tena Oktoba 28,2017 timu hizo zilipotoka sare ya bao 1-1.

Dar es Salaam.Mshambuliaji wa Simba,Shiza Kichuya amesema bao lake la kwanza lilofunga msimu huu dhdi ya African Lyon litamfungulia njia ya kufunga mengine zaidi.
Kichuya ameanza msimu vibaya huku  akionekana kushuka kiwango jambo lililosababisha akachwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania'Taifa Stars.
Kichuya alisema alikuwa akitafuta sana nafasi ya kufunga ili apate morali ya kufanya vizuri zaidi na anashukuru ametimiza jambo hilo Oktoba 6 mwaka huu alipofunga bao moja katika ushindi ya mabao 2-1 ilioupata Simba dhidi ya African Lyon.
"Kufunga inategemea na nafasi unayopata lakini wengi hawajui kuwa wakati mwingine kocha ananipa majukumu tofauti hivyo  nakuwa sina nafasi kubwa ya kufunga kama wengi wanavyotaka.
"Nafurahi nimefunga bao langu la kwanza msimu huu na naamini bao hilo litanipa morali ya kuendelea kufunga zaidi pale nitakapopata nafasi ya kufanya hivyo.
Kichuya alisema ligi ya msimu huu ni ngumu lakini anaamini watatetea ubingwa wao licha ya kwamba wako nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.
"Ligi imekuwa ngumu msimu huu lakini nafasi ya kutetea ubingwa wetu ipo tena kubwa muhimu ni kila mchezaji kuongeza juhudi na kutimiza majukumu yake ipasavyo"alisema Kichuya.