Kamusoko awatuliza Yanga kombe la FA,awaita Kirumba
Muktasari:
Kwa sasa kikosi hicho chini ya Kocha wake raia wa DR Congo,Mwinyi Zahera kinapambana vikali katika mechi zake za Ligi Kuu na FA ili kuweza kushiriki kimataifa.
KIUNGO wa Yanga,Thaban Kamusoko amesema kuwa pamoja na ugumu wa mechi ya kesho Jumamosi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Alliance FC lakini hawana hofu juu ya ushindi na kwamba wamedhamiria kubeba Ubingwa wa michuano hiyo.
Yanga ambayo ilitua jijini hapa juzi asubuhi kwa usafiri wa Ndege ya Shirika la Air Tanzania,jioni yake walijifua kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba ili kujiweka sawa.
Mabingwa hao wa kihistoria,msimu huu hawakuwa na ushiriki wowote wa michuano ya kimataifa,baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu uliobebwa na Simba na ule wa Kombe la Shirikisho ulioenda kwa Mtibwa Sugar.
Soma hapa zaidi>>Yanga yajiandaa kumalizana na Alliance
Kwa sasa kikosi hicho chini ya Kocha wake raia wa DR Congo,Mwinyi Zahera kinapambana vikali katika mechi zake za Ligi Kuu na FA ili kuweza kushiriki kimataifa.
Akizungumza baada ya mazoezi yao,Kamusoko alisema kuwa mchezo wao wa leo utakuwa mgumu lakini kutoka na morari waliyonayo pamoja na dhamira yao kwenye michuano hiyo lazima washinde.
Alisema kuwa pamoja na kuwakosa baadhi ya nyota wenzao ambao kimsingi wangesaidia chochote,lakini hata waliopata bahati ya kuungana na timu watafanya vizuri.
“Tunawakabiri Alliance kwa tahadhari lakini kwa kujiamini,tuliwafunga mechi ya mwisho tuliyokutana nao kwahiyo kikubwa ni kupambana kila mmoja wetu ili kutimiza malengo”alisema Kamusoko.
Kwa upande wake Winga wa kushoto,Jafary Mohamed alisema kuwa kutokana na maandalzi waliyoyafanya lazima wafanye kweli na kwamba wanawaheshimu Alliance lakini hawawaogopi.
“Ushindi uko palepale kimsingi mashabiki wetu waje kwa wingi kutusapoti,mechi hii ni muhimu sana kwetu katika kusaka nafasi ya kusonga Nusu Fainali ya michuano hii’alisema Mohamed.