Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KARIAKOO DABI: Zahera aanza na pumzi Moro

Muktasari:

Simba na Yanga zinakutana Septemba 30 ikiwa ni mechi ya  101 katika historia yao

Morogoro: Yanga imeendelea na mazoezi katika siku ya pili leo hapa Morogoro lakini kocha wa timu hiyo ameanza na kurudisha pumzi.
Asubuhi leo Jumatano, Yanga wanafanya mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri, ambapo kocha    Mwinyi Zahera ameonekana akianza na mazoezi ya kuongeza pumzi.
Katika mazoezi hayo Zahera ameonekana akiwawanya wachezaji wake katika makundi mawili moja likisimamiwa na mwenyewe huku lingine likisimamiwa na msaidizi wake, Noel Mwandila.
   Kocha Zahera ameonekana kutaka kuona mchezaji anakimbia kwa kufuata muda aliotaka yakiwa ni mazoezi ya mbio za kasi.
Kila mchezaji alihidhuria mazoezi hayo isipokuwa makipa pekee ambao walikuwa na mazoezi yao na kocha wao Juma Pondamali.
Mpaka sasa Yanga inaonekana haina mchezaji majeruhi ukiondoa Juma Abdul na Juma Mahadhi ambao bado hawajajiunga na timu hiyo.