Fei Toto hana presha Yanga

Friday February 14 2020

Fei Toto hana presha Yanga,KIUNGO wa Yanga, Fei Toto ,Kukaa benchi kwa Fei Toto ,

 

By Olipa Assa

KIUNGO wa Yanga, Fei Toto amesema ana tabia za kudhamiria ndoto yake hata kama anapitia changamoto lakini huwa anaamini ipo siku atafanikiwa kufikia anapopataka.

Fei Toto kwa sasa hapati nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha Yanga, amesema hilo haliwezi kufifisha ndoto yake kwenda kucheza nje.

"Unajua kuna watu wanaona kama nimeridhika na kuishia kucheza soka la Bongo, bado nina ndoto kubwa na ipo siku itakuja kujidhihirisha wazi na wataamini ninachokisema kwa sasa,"amesema.

Kuhusu kutocheza ndani ya kikosi cha kwanza cha Yanga, amesema anaichukulia kama changamoto ya kuendelea kupambana kuboresha kiwango chake.

"Ushindani wa namba unafanya kikosi kiwe imara, naufurahia kwani nikipata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kama msimu ulioisha, naamini wale ninaocheza nao nafasi yangu na wao wataongeza bidii kwa faida ya timu,"amesema.

Advertisement