Fei Toto: Ndoto yetu imetimia kucheza kimataifa

Muktasari:

  • Staa wa Yanga afurahia fursa ilioipata timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa kwa mwaka huu.

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema klabu hiyo kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa mwaka huu ni faraja kwa mashabiki wao ambao walikuwa na hamu kuona jambo hilo.
Fei Toto anayehusishwa kutaka kutimkia nje kucheza soka la kulipwa, anasema hiyo ni nafasi adimu kwa Yanga baada ya ndoto zao kugonga mwamba katika ligi iliyomalizika hivi karibuni ambapo walishindwa kuchukua ubingwa.
"Kila mdau aliona namna ambavyo Yanga tulikuwa tumepambana kwa nguvu zetu zote kuchukua ubingwa, ilishindikana tukaishia nafasi ya pili.
"Hamu yetu ilikuwa ni kushiriki michuano ya kimataifa, lakini kwa kuwa limetokea hili ni jambo la heri kwa klabu yetu pia faraja sana kwa mashabiki kuona timu yao ina majukumu ya kimataifa.
"Yanga na Simba zina ushindani wa hali ya juu, ndio maana timu hizo mahesabu yao ni ubingwa inapotokea mmoja wapo hajafanikiwa kutwaa taji hilo basi mashabiki wanakuwa na maumivu makubwa"anasema.