Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dalali aita wanachama kutoa baraka za msimu ujao

Muktasari:

Dalali amesema wanachama wakijitokeza kwa wingi itasaidia kila mmoja kwa imani yake kukibariki kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu na kwamba utakuwa na ushindani mkubwa.

MWANZILISHI wa Simba Day na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali ametoa neno kuelekea tamasha hilo, litakalofanyika Jumanne ya wiki ijayo, kwamba wanachama wajitokeze kwa wingi kuwatakia baraka wachezaji wao.
Simba Day ilianzishwa chini ya Dalali mwaka 2009 na imekuwa ikiendelezwa na kila kiongozi anayeingia madarakani.
Dalali amesema wanachama wakijitokeza kwa wingi itasaidia kila mmoja kwa imani yake kukibariki kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu na kwamba utakuwa na ushindani mkubwa.
"Lengo  kuu la Simba Day, nikutambulisha silaha zetu za kufanya kazi kwa msimu mpya ili kujuana na wanachama baada ya kuwasikia kwenye usajili, hapo watapata baraka zote kwa Wanasimba.
"Kukusanya pesa za kujenga uwanja, kutambulisha jezi za wachezaji, kurudisha shukrani kwa jamii kwa maana ya wale ambao wanatuunga mkono katika kazi zetu kufanya kitu kwa ajili yao," amesema.
Dalali amesema kuna haja kwa wanachama wa Simba kutoka mikoa yote ya Tanzania kuungana kwa pamoja kuhakikisha wanafanya kitu kwa ajili ya siku hiyo, aliodai ni muhimu  kwa ajili ya kuandaa mikakati itakayowafanya watetee ubingwa.
"Kila klabu ina utaratibu wake, Simba tuna siku ya Simba Day ambayo wiki nzima tunakuwa tunafanya vitu mbalimbali vya kijamii ambavyo  sasa tutahitimisha kwa pamoja na kuwatakia kila raheli wachezaji wetu kutimiza majukumu ya klabu,"amessema.
MOGELLA ACHAMBUA JEZI
Kuna ishu inaendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na jezi ambazo zitatumiwa na klabu hizo kwa msimu ujao, huku rangi ya pinki ya uzi wa Simba ikionekaba kubezwa, katika hilo staa wa zamani wa timu hiyo,Zamoyoni Mogella ametia neno.
Mogella amesema maisha yanabadilika akidai kwamba asili yao zamani jezi za Simba ilikuwa na rangi nyekundu na nyeupe, akisisitiza kinachoendelea kwa sasa hakishangai.
"Simba na Yanga zina tamaduni zake kama mambo yanabadilika hatuna budi kuyafuata kwani kuiga sio dhambi, kikubwa wachezaji wakaonyeshe uwezo uwanjani na sio rangi mara pinki mara nyekundu.
"Yanga nao hata kama wanataniwa kuona jezi zao za juu kama blauzi, wala wasijali wanachotakiwa wachezaji wao ni kucheza soka la ushindani hiyo ndio pointi yao ya msingi kwani mwisho wa siku ndio wanaotegemewa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania," amesema Mogella.