Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkwabi: Nimefanya uamuzi wa kishujaa kuondoka Simba

Muktasari:

Mkwabi ambaye alidumu madarakani kwa miezi 10 tangu alipochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu Novemba mwaka jana, ameliambia Mwanaspoti amejiuzulu ili kutoa mwanya wa klabu hiyo kufikiria maendeleo badala ya kufikiria ugomvi na unafiki wa baadhi ya viongozi.

Dar es Salaam. SIKU chache baada ya kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Swedy Mkwabi amesema amefanya uamuzi wa kishujaa kuachia wadhifa huo huku akisema unafiki ndio umemwondoa.
Pia, amewataka wanachama wa Simba kuendelea kuipa sapoti timu yao ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa makini kinachoendelea ndani ya klabu hiyo.
Mkwabi ambaye alidumu madarakani kwa miezi 10 tangu alipochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu Novemba mwaka jana, ameliambia Mwanaspoti amejiuzulu ili kutoa mwanya wa klabu hiyo kufikiria maendeleo badala ya kufikiria ugomvi na unafiki wa baadhi ya viongozi.
Hivi karibuni taarifa iliyotolewa na Simba ilieleza Mkwabi amejiuzulu ili kupata muda zaidi wa kusimamia shughuli zake binafsi.
“Naamini nimefanya uamuzi wa busara na wa kishuja kukaa pembeni Simba, huu sio wakati wa klabu kufikiria masuala ya ugomvi badala ya maendeleo, hivyo ili wasifikirie ugomvi zaidi na kusahau maendeleo, nimeona nifanye busara kukaa kando.
“Ingawa kinachoendelea ndani ya klabu ya Simba kwa sasa kama hakutakuwa na mabadiliko, basi muda ndiyo utazungumza na ukweli utajulika siku si nyingi,” alisema.
Hata hivyo, Mkwabi licha ya kujiuzulu amesema muda aliodumu madarakani Simba, anajivunia mambo makubwa manne aliyoshiriki kikamilifu kuyafanya na yatabaki kuwa alama kwenye uongozi wake.
“Kikubwa ninachojivunia ni kuwa miongoni mwa walioiongoza Simba kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita pamoja na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo.”
Hata hivyo, alisema licha ya mafanikio hayo, jambo kubwa lililomkwaza kwenye uongozi wake katika kipindi chote akiwa Mwenyekiti wa Simba ni unafiki wa baadhi ya viongozi.
“Unafiki katika mpira upo sana, simaanishi katika Bodi ya Wakurugenzi pekee, lakini nazungumzia ‘general’ unafiki ni jambo ambalo limenikwaza kipindi cha uongozi wangu na nitaendelea kulichukia.”
Alisema katika uongozi wake alipenda zaidi  ukweli na uwazi kwenye mambo yanayohusu klabu, lakini alichojifunza katika mpira, mtu mkweli na anayesimamia masilahi ya wengi huwa hapendwi.  Hata hivyo, Mkwabi alisema hajafikiria kama miaka ijayo atarudi kugombea ili kuongoza klabu hiyo ambayo baada ya kujiuzulu anaendelea kuitumikia kama mwanachama wa kawaida.
Lakiani, baada ya Mkwabi kuachia wadhifa huo kumekuwa na taarifa aliyekuwa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah (Try Again) amekuwa akitajwa kurithi nafasi hiyo. Taarifa kutoka mitaa ya Msimbazi, zinaeleza Try Again ambaye aliiongoza Simba kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko, amekuwa akishawishiwa na baadhi ya wanachama na wengine wakiahidi kumchukulia fomu muda ukifika. Hata hivyo, mwenyewe amezungumza na Mwanaspoti na kueleza kwa sasa hana mpango huo.
Try Again alisema mchakato wa kujaza nafasi ya Mkwabi unapaswa kukamilika ndani ya miezi mitatu tangu alipojiuzulu.
Hata hivyo, alisema Simba inaweza kujiongoza bila kuwa na mwenyekiti kwa kuwa, imeingia kwenye mfumo mpya unaoitambua kama taasisi ama kampuni na Mtendaji Mkuu ndio mtendaji wa shughuli za kila siku huku bodi ikikutana mara chache.

Rage, Mwameja, Mogella wafunguka
Kwa nyakati tofauti, nyota wa zamani wa Simba, Mohammed Mwameja, Zamoyoni Mogella na Ismail Aden Rage aliyewahi pia kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo walizungumzia uamuzi huo wa Mkwabi.
“Mkwabi yuko sahihi, hata ushauri wake kwa wanachama kufuatilia kinachoendelea ndani ya klabu ni sahihi na ni haki yao,” alisema Mogella mshambuliaji nyota wa zamani wa Simba na mwanachama wa klabu hiyo na kuongeza. “Mkwabi amesema ukweli kuhusu unafiki katika soka upo hasa nyakati hizi na baadhi yetu wanapatia riziki zao huko, ameona mbali.”
Mwameja kipa wa zamani wa timu hiyo alisema suala la kujuzulu kwa Mwabi bado linawaumiza vichwa watu wengi. “Siwezi kuchangia chochote sasa, lakini wanachama wengi walimpenda kwa misimamo yake mengi tuyaache kwanza,” alisema.
Rage alisema atatoa maoni yake kuhusu ushauri huo wa Mkwabi kwa wanachama atakaposoma kwanza kile alichokisema. Simba hivi sasa imeingia katika mfumo wa kujindesha kwa hisa na wanachama wanamiliki asilimia 51 na mwekezaji asilimia 49.