Mayay: Moro, Sonso sawa ila hakuna kama Yondani

Muktasari:

Kocha Mwinyi Zahera alimuanzisha Moro na Sonso waliosajiliwa Yanga msimu huu. Yondani, Andrew Vincent walikuwa timu ya Taifa.

Dar es Salaam.Licha ya mabeki wapya wa Yanga, Lamine Moro na Ally Sonso kucheza kwa kiwango bora katika mchezo wao wa kwanza wa kimataifa katika kikosi cha Yanga, Ally Mayay anaamini hakuna beki wa kumuweka benchi Kelvin Yondani.
Kocha Mwinyi Zahera alimuanzisha Moro na Sonso waliosajiliwa Yanga msimu huu. Yondani, Andrew Vincent walikuwa timu ya Taifa.
Hata hivyo, uwezo wa mabeki hao unaonyesha dalili za kuwepo kwa ushindani wa namba kati ya mabeki hao katika kikosi cha kwanza.
“Dante, Moro na Sonso  itabidi wapokezane kuanza, lakini kwa Yondani bado namuona ana namba ya kudumu Yanga,” alisema Ally Mayay ambaye pia ni mchambuzi wa soka nchini. Alisema Yondani ana nafasi ya kudumu katika safu ya ulinzi ana vitu vingi kulinganisha na wenzake uwanjani.
“Achana na uzoefu wake wa muda mrefu, bado ataendelea kuwa kiongozi kwa wenzake hata kama si nahodha tena wa timu hiyo.
“Yuko fiti, ana uwezo mkubwa uwanjani na ni mzoefu hivyo sioni sababu ya kugombea namba.  Akina Moro watabadilishana namba lakini si Yondani,” alisema Mayay.