Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bigirimana aikacha APR kweupe, Kalengo ajitosa jumla Yanga

Muktasari:

Usajili huo wa Kalengo unaifanya Yanga kunasa vifaa sita mpaka sasa wakiwemo mawinga Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, beki Lamine Moro na kiungo mkabaji Abdulaziz Makame

YANGA imekamilisha usajili wa mashine tano zilizotua safu ya ushambuliaji, lakini pia kiungo wao mpya Issa Bigirimana amewacheka viongozi wake wa APR, akisema sasa maisha yake yako Yanga.
Tuanze na yule aliyesaini juzi usiku kama ambavyo Mwanaspoti lilikuarifu mapema tu kuwa Yanga ilimshusha straika wake mpya Kalengo Maybin akitokea Zesco na tayari amesaini.
Kalengo, ambaye ni ndugu wa mkongwe wa soka la Zambia, Winston Kalengo alisaini mkataba wa miaka miwili kuvaa jezi za Jangwani.
Mkataba huo umesainiwa juzi usiku kwenye Makao Makuu ya Yanga, Jangwani, kisha akachukua zake ndege haraka kumalizia majukumu yake akiwa na Zesco inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, George Lwandamina ‘Chicken’.
Hata hivyo, habari zinaarifu kuwa ujio wa Kalengo ndani ya Yanga ni kazi ya Lwandamina akishirikiana na kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila.
Usajili huo wa Kalengo unaifanya Yanga kunasa vifaa sita mpaka sasa wakiwemo mawinga Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, beki Lamine Moro na kiungo mkabaji Abdulaziz Makame

Bigirimana achomoa
Juzi na jana kulikuwa na taarifa kwamba, mabosi wa APR wameishangaa Yanga kumsainisha Bigirimana, lakini mwenyewe amefunguka akisema hana mkataba na wababe hao wa soka la Rwanda.
Katibu Mkuu wa APR, Adolph Kalisa alinukuliwa akisema wanashangazwa na Yanga kumnasa mchezaji wao, ambaye bado ana mkataba hadi mwaka 2020 na kwamba, watachukua hatua za kisheria.
Lakini, Bigirimana amezungumza na Mwanaspoti na kueleza kuwa APR imepandwa hasira baada ya uamuzi wake wa kusaini Yanga kwani walikuwa kwenye mchakato wa kumpa mkataba mrefu zaidi. “Unajua huku Rwanda mashabiki wamechukia kuona naondoka, APR walitaka kunipa mkataba mrefu na nikawaambia wasubiri kwanza nimalizane na mechi iliyobaki,” alisema.
Alisema kwa sasa mkataba wake na APR ambao umebakiza siku chache kumalizika hapo ndipo utakuwa mwisho wa maisha yake kwa wababe hao.
“Niliamua kutulia kwanza ili kuona mazungumzo na Yanga yataishia wapi, lakini tumemaliza vyema na nimesaini mkataba wa kufanya kazi,” alisema na kuongeza:
“Mabosi wa Yanga waliniuliza mapema kuhusiana na mkataba wangu na nakala ninazo hapa. Viongozi wa APR wamepatwa hasira, hivyo Yanga wasihofu mimi ni mchezaji wao.”
Pia, alisisitiza kuwa hata Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) linafahamu kuhusiana na mkataba wake kwa kuwa kuna nakala halisi.
Mabosi wa Yanga mpaka sasa hawajatoa tamko lolote kuhusiana na mkwara huo wa APR, hata alipotafutwa Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela simu yake iliita bila majibu.