Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okwi atimka Simba unaambiwa

Muktasari:

Msimu uliopita Okwi alikuwa kinara wa mabao katika Ligi akifunga 20 na Kombe la Shirikisho Afrika alifunga matatu, japo msimu huu tayari ana mabao saba katika Ligi Kuu na hajafunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika

Dar es Salaam. Mashabiki wa Simba wajiandae kupata mshtuko, kwani nyota wao Emmanuel Okwi anahesabu siku kabla ya kutimka Msimbazi, baada ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kutoa ofa kwa straika huyo kutoka Uganda.
Mwanaspoti ilipata taarifa za uhakika kuwa viongozi wa  Kaizer Chiefs ambao wapo Zanzibar kuvaana na Zimamoto wanamtaka Okwi na wanasubiri mkataba wake tu ili ambebe.
Okwi alijiunga na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na kumalizika mwishoni mwa msimu na mabosi Kaizer wanamtaka kiulaini ili akaichezea timu yao katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
Kaizer Chiefs ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 14 tayari imewasilisha ombi kwa Simba ili wawachie Okwi kwa dau lolote watakalokubaliana na kama itashindikana watamsubiri hadi mkataba umalizike.
Msimu uliopita Okwi alikuwa kinara wa mabao katika Ligi akifunga 20 na Kombe la Shirikisho Afrika alifunga matatu, japo msimu huu tayari ana mabao saba katika Ligi Kuu na hajafunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika.