Aussems kumfikisha mbali Mo Ibrahim
Muktasari:
Kila kocha ana jicho lake la kuona kama ilivyo kwa Aussems wa Simba, kuona kitu kwa Mo Ibrahim anayempa nafasi ya kucheza tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita kwa Lachantre.
KIUNGO wa Simba, Ibrahim Mohamed 'Mo Ibrahim' ameanza kurejea kwenye makali yake baada ya kupata nafasi mbele ya kocha Patrick Aussems, kitu anachokiamini kitampa hatua kubwa.
Katika msimu wa 2017/18 Mo Ibrahim, kiwango chake kilionekana kuyumba baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pierre Lachantre kukiri mchezaji huyo hana nidhamu ya kazi inayofanya ashindwe kumwamini kwenye kikosi chake cha kwanza.
Mo Ibrahim amezungumzia nafasi anayoipata kama inamrudisha kwenye mstari wa ndoto zake , akiamini ana uwezo isipokuwa anahitaji kuongeza bidii.
"Mchezaji akiwa fundi ni fundi tu, mengine yanakuja kwa wakati, natambua kwamba kujituma na bidii ni kazi yangu, hivyo naamini kufanya kitu cha kitofauti kwenye msimu wa 2018/19,"anasema.