Mzee Akilimali aridhia kikao maandalizi ya uchaguzi
Muktasari:
Mwakyembe amesema baaada ya kuzisikila pande zote amewaambia kwamba msiimamo juu ya uchaguzi huo utatolewa baada ya siku mbili. Amesema ameomba muda huo ili aweze kukutana na baadhi ya watendaji wa TFF na serikali kuweza kutoa muongozo wa serikali.
Kikao cha wanachama wa Yanga kutoka makundi yanayovutana juu ya uchaguzi mkuu wa Yanga itajulikana baada ya siku mbili.
Kikao hicho ambacho kiliitishwa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kimemalizika na baadhi ya wanachama wakiridhishwa na kilivyoendeshwa.
Dk Mwakyembe amesema licha ya mvutano wa wanachama hao lakini kikao hicho kimekuwa na mafanikio makubwa.
Mwakyembe amesema baaada ya kuzisikila pande zote amewaambia kwamba msiimamo juu ya uchaguzi huo utatolewa baada ya siku mbili.
Amesema ameomba muda huo ili aweze kukutana na baadhi ya watendaji wa TFF na serikali kuweza kutoa muongozo wa serikali.
Aidha Mwakyembe amewaambia wanachama hao pamoja na viongozi wao kwamba serikali haitaki kuona Yanga inatetereka hasa wakati huu ambao wanafanya vizuri katika Ligi Kuu Bara
Aidha Mzee Ibrahim Akilimali ambaye alishiriki kikao hicho amesema wameridhika na kikao hicho wanasubiri maamuzi wa Waziri Mwakyembe.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omari Kaya amesema wameridhika na uendeshwaji wa kikao hicho na sasa wanasubiri muongozo.