Aussems alia na viwanja vibovu ligi kuu

Muktasari:

Kocha wa Simba, Aussems kwa muda mrefu ametajwa kuwa kwenye mgogoro na msaidizi wake Masoud Djuma lakini hivi karibuni makocha hao walionekana wakiwa kwenye bechi wakijadiliana kana kwamba hakuna kitu kilichokuwa kinaendelea. Hata hivyo masoud Djuma tayari ameachana na klabu hiyo ya Msimbazi.

Kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema hana wasiwasi na timu  aliyonayo lakini changamoto kubwa ni viwanja vya mikoani.
Aussems amesema hawezi kubadili aina ya soka la pasi ambalo Simba inacheza lakini malengo yao ya ushindi yanakumbana na hali ya viwanja vibovu.
Kocha huyo amesema ili soka la Tanzania lipige hatua linahitaji viwanja vizuri kuruhusu kila kila timu kucheza soka inalotaka.
Amesema anawashukuru viongozi wa klabu yake kwa akili ya kuanza kujenga uwanja wa mazoezi ambao utaisaidia klabu yao.
Amesema katika mechi alizocheza nje ya jiji la Dar kutofanya vizuri kama walivyotarajia kulitokana na hali mbaya ya viwanja.