Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbelgiji akomalia nyota 13

KIKOSI cha Simba, kesho Jumatano kitavuka Bahari ya Hindi kwenda Zanzibar tayari kuwasha moto katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, huku Kocha Patrick Aussems akiamua kukomaa na wachezaji 13 ambao hawakupewa mapumziko kama wenzao.

Kocha huyo kutoka Ubelgiji aliamua kuwapa nyota wake wa kikosi cha kwanza mapumziko mafupi ya siku tatu, huku akikomaa na wengine walioshindwa kuibeba timu hiyo mbele ya Mashujaa FC kwenye mechi yao ya Kombe la FA.

Wachezaji waliokuwa mapumziko wataungana na wenzao hao 13 leo Jumanne kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kupanda boti kuelekea Zanzibar kutesti zali kwenye Mapinduzi 2019.

Wachezaji hao 13 waliokuwa wakipigishwa tizi Gym iliyopo hoteli wanayoweka kambi timu hiyo na Kocha wa Viungo, Adel Zrane ili kuwekwa fiti ni pamoja na Deogratius Munishi ‘Dida’, Ally Salim, Zana Oumar Coulibaly, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yusuf Mlipili, Paul Bukaba, Mohammed Ibrahim, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Abdul Selemani, Adam Salamba na Haruna Niyonzima.

Kocha Aussems alisema aliamua kuwapigisha tizi wachezaji hao kama mpango wa kuiandaa timu yake kwa ajili ya mechi ngumu inayowakabili mbele hasa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria itakayochezwa Januari 11 kwenye Uwanja wa Taifa.

“Wanaendelea kufanya mazoezi ni kama sehemu ya maandalizi ili kuwa sawa katika hali ya kushindana kama wale ambao niliwatumia ili yoyote atakayepata nafasi katika hizi mechi ngumu za Kimataifa afanye kitu atakachotakiwa kufanya.”

“Wachezaji wote watakutana kesho (leo Jumanne) na Jumatano tutakwenda Zanzibar kwa michuano ya Mapinduzi, tutayatumia kama sehemu ya maandalizi ya mechi yetu ya kimataifa. Tutacheza mechi za Januari 4 na 6, lakini ikifika Januari 8 nataka timu iwe Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mechi na JS Saoura.” alisema.

Kocha Aussems alisema anajivunia kucheza mechi ya kwanza uwanja wa nyumbani na kuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kuipa nguvu timu na kuishangilia akiamini kutawasaidia kupata ushindi katika mchezo huo mgumu.

Naye beki Mlipili alisema wanayatumia mazoezi hayo kujiweka fiti kwa mechi za Mapinduzi akiahidi kurejesha heshima yao kwa mashabiki na kula sahani moja na wenzao walio fiti zaidi kikosini.

“Mapinduzi yaweza kuwa michuano kwetu kwa tusiopata nafasi ya kucheza Ligi Kuu kwa kuonesha kiwango chetu na kumshawishi Kocha,” alisema Mlipili.