Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zahera ataja matatu yanayoharibu hadhi ya Ligi Kuu

Muktasari:

Kocha Zahera amesema kama Shirikisho la Soka Tanzania itayafanyia kazi haya ligi inaweza kuwa na ushindani mkubwa na kukuza soka la Tanzania.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuna mambo matatu yanayoondoa hadhi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kocha Zahera amesema ukosefu wa fedha kumudu uendeshwaji wa ligi jambo la kwanza kubwa linaloharibu ubora wa ligi kutokana na klabu nyingi kuishi maisha ya shida.

"Klabu zinasafiri umbali mrefu kuna timu nyingine zinatumia mabasi madogo wanajikunja wakifika wamechoka, kutokana na kukosa fedha zinalazimika kusafiri na wakifika kesho yake wanatakiwa kucheza mechi kuhofia gharama za malazi,” amesema Zahera

Zahera amesema eneo la pili ni mgawanyo mbovu wa mapato ambapo kutokana na ligi kukosa udhamini mfumo wa mgawayo wa mapato ni lazima ubadilishwe kwa kila klabu kuambilia kitu katika mechi inazocheza tofautio na sasa kuwa timu mwenyeji anachukua mapato yote.

"Huu mfumo wa sasa klabu mwenyeji kuchukua mapato yote ni lazima ubadilishwe hasa wakati huu hakuna mdhamini wa ligi timu inacheza mechi inatumia sh 30 milioni ikimaliza mechi haipati hata shilingi moja.

Amesema eneo lingine ni ubovu wa viwanja ambapo kuna baadhi ya viwanja havifai kuchezewa mechi za ligi kutokana na ubora mdogo.

"Kuna viwanja vibovu sana uwanja kama ule wa Singida,uwanja kama ule wa Morogoro,Shinyanga ni viwanja vibovu sana havifai kuchezewa ligi kama shirikisho linataka maendeleo ya soka ni lazima wasimamie haya yarekebishwe."