Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zahera amvua unahodha Yondani ampa Ibrahim Ajibu

Muktasari:

Kelvin Yondani alilirithi kitambaa cha unahodha kutoka kwa aliyekuwa beki wa kati, Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye alistaafu na kupewa kazi ya umeneja katika kikosi hicho.

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera amemvua unahodha beki wa kati, Kelvin Yondani 'Vidic' kutokana na utovu wa nidhamu.
Yondani ambaye mwanzoni mwa msimu huu alitangazwa rasmi kuwa nahodha wa Yanga akibeba mikoba iliyoachwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye pia alikuwa anacheza nafasi ya beki wa kati, amevuliwa wadhifa huo kutokana na kuchelewa mazoezini pamoja na ukimya.
"Niliwapa wachezaji siku tano za mapumziko ili siku ya sita waje mazoezini yeye hakutokea, amezima simu na amegoma.
Siwezi kumwacha mtu kama yule anayepaswa kuonyesha mfano kwa wengine afanye hayo hivyo nimeamua nimvue unahodha na kuanzia sasa  nahodha ni Ibrahim Ajibu,"alisema Zahera ambaye ni kocha mwenye msimamo na anachokizungumza.
Ikumbukwe pia, Zahera alifanya maamuzi ya kumkataa kikosini mwake mlinda mlango, Beno Kakolanya kwa matatizo kama hayo na mpaka sasa hajajiunga na timu.