Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zahera aitangazia kiama Mbeya City

Muktasari:

  • Chini ya Zahera, Yanga imepata ushindi kwenye mechi zote ilizocheza mikoani msimu huu wa Ligi Kuu dhidi ya timu za African Lyon, Prisons, Kagera Sugar na Mwadui FC.

MBEYA. Kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema klabu hiyo ataendeleza historia ya kuondoka na ponti tatu mikoani pale wanapokutana na timu pinzaniwakati watakaupokutana na Mbeya City kesho.
Zahera ametamba hivyo leo baada ya kumaliza kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
“Sisi mwendo wetu ni uleule  wa kuondoka na pointi tatu ni kila mechi tutakayocheza. Yote hiyo ni kwa sababu kikosi changu ni kizuri hivyo nawaomba mashabiki wa Yanga waje kwa wingi  na kushuhudia tunaitandika Mbeya City kwenye uwanja wao wa nyumbani”, alisema Zahera.
Zahera ameongeza kuwa anatarajia kuona marefa watakao chezesha mchezo wao wa kesh watakuwa na weledi wa hali ya juu katika kutafsiri sheria  za mpira wa miguu.
Hata hivyo Zahera amesema katika mchezo wa kesho anatarajia kumchezesha Haruna Moshi maarufu Bobani kutokana kupendezwa na mchezo wake aliyouonyeshwa wakati wa mechi ya Tukuyu star uliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.