Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga inamuhitaji zaidi Manji kuliko Manji anavyotaka

Muktasari:

Robert Ekerege aliwahi kuwa Meneja wa Yanga miaka ya nyuma ni miongoni mwa wanachama waliomshawishi Yusuf Manji kuingia ndani ya Yanga kwa mara ya kwanza Manji alitoa Sh 2.4 milioni wakati timu hiyo ilikuwa inakwenda kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba, mwaka 2005.

Dar es Salaam.MENEJA wa zamani na mwanachama wa Yanga, Robert Ekerege ameibuka na kuwaambia Wanayanga kwamba hakuna namna nyingine ya kumaliza matatizo ya kifedha ndani ya klabu yao zaidi ya uwepo wa Yusuf Manji kwasasa.
Hivi sasa Yanga wapo kwenye mchakato wa uchaguzi ingawa bado kuna mvutano kati ya klabu hiyo na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambao sasa ndiyo wanaendesha mchakato huo kwa maagizo ya serikali kwamba wasimamie kwa vile Kamati ya Utendaji ya Yanga haijatimia kwani  wajumbe wengi walijiuzulu.
Yanga wanamuhitaji Manji ambaye mwaka jana aliandika barua ya kujiuzulu ambapo wanachama waligoma na kwamba wanamtambua kama Mwenyekiti wao na awali TFF ilibariki maamuzi hao ya wanachama wa Yanga ingawa sasa hawatambui na kuwataka nafasi yake ijazwe kupitia uchaguzi huo.
Ekerege aliliambia Mwanaspoti kuwa wanachama na wadau wengi hawafahamu undani wa tatizo la Yanga kwani hivi sasa hakuna mtu ambaye anaweza kuingia Yanga na kulipa madeni yote hasa ya wachezaji wao, kwani waliowengi uwezo wao ni wa kawaida na hawapo tayari kujitolea.
"Manji hana nia ya kukaa Yanga milele, jambo pekee ambalo wanapaswa kulifahamu ni kwamba uwepo wa Manji utaisaidia klabu kuvuka kwenye kipindi hiki kigumu ikiwemo kutusaidia kusajili wachezaji wa maana vinginevyo hizi propaganda zikiendelea itakula kwetu, dirisha la usaliji litafungwa tutabaki hivi hivi.
"Manji amekubali kurejea Yanga na sio kwamba anahitaji kiivyo kukaa Yanga na uhitaji wake ni tofauti na Yanga inavyomuhitaji Manji na hiyo yote ni kwavile amekuwa na msaada mkubwa ndani ya Yanga.
"Waruhusu Manji afanye kazi yake kwa miaka miwili ijayo wakati tunajipanga, muda ukifika wa kufanya uchaguzi tutafanya kwani akiwa anaendelea na madaraka yake tutakuwa tunaendelea na mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji maana hiyo ndiyo njia pekee ya kujikwamua, hata yeye ndiyo malengo yake," alisema Ekerege.
Uchaguzi wa Yanga unatarajia kufanyika Januari 13 mwakani huku wagombea zaidi ya 20 wakijitokeza kuchukuwa fomu nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.