Wanawake wanavyojishindia mamilioni kupitia SportPesa
Muktasari:
- Washindi hao ambao ni Grace George Litimba na Husna Dauda Abubakari, wamekuwa ni moja ya simulizi kubwa ya wanawake kujishindia mamilioni kupitia SportPesa.
SportPesa Tanzania inasherehekea mafanikio makubwa baada ya wanawake wawili kutoka mazingira tofouti kushinda jumla ya Sh 857 milioni, jambo linaloonyesha kukua kwa ushiriki wa kinamama katika michezo ya kubahatisha nchini.
Washindi hao ambao ni Grace George Litimba na Husna Dauda Abubakari, wamekuwa ni moja ya simulizi kubwa ya wanawake kujishindia mamilioni kupitia SportPesa.
Grace aliandika historia baada ya kujishindia Sh 400 milioni kupititia mchezo wa Aviator, na kuwa mshindi mkubwa zaidi wa Aviator kuwahi kurekodiwa nchini Tanzania hadi leo hii.
Grace, ambaye ni mwalimu, mfanyabiashara na mama mwenye umri wa zaidi ya miaka 50, ambaye muda wake mwingi anautumia kwenye familia, kazi ya ualimu pamoja na biashara zake, alipata nafasi ya kuuzungumzia ushindi huo aliopata akisema fedha hizo zitamsaidia kuongeza uwekezaji, kukuza biashara na kusaidia familia.
“Ushindi huu umebadilisha kabisa maisha yangu. Nataka kufanya uamuzi sahihi kwa ajili ya maisha yangu ya baadaye kwa kuongeza uwekezaji, kukuza biashara na kusaidia familia yangu,” alisema.
Wakati simulizi ya Grace ikifuatiliwa na watu wengi nchini, mwanamke mwingine ametengeneza historia nyingine ya kuvutia kupitia SportPesa Supa Jackpot.
Husna mwenye umri wa miaka 36, mfanyabiashara kutoka Kibaha na shabiki mkubwa wa Yanga, hivi karibuni alijishindia Sh457,989,839 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 14 za SportPesa Supa Jackpot.
Mwanamama huyo ambaye pia ni mama wa mtoto mwenye mwezi mmoja, aliambatana na mume wake pamoja na familia alipofika kuchukua ushindi wake katika ofisi za SportPesa Tanzania, jambo lililogeuza tukio hilo kuwa furaha ya pamoja kwa watu waliokuwa wakimuunga mkono katika safari yake.
“Nilipoona matokeo kwa mara ya kwanza, kwa kweli sikuamini. Nilikua nikiyaangalia tena na tena kwa sababu kushinda kiasi hiki ilikuwa ni ndoto kwangu. Huu ni ushindi ambao umebadilisha maisha yangu na familia yangu kwa ujumla,” amesema.
Husna ambaye ni mchezaji wa mara kwa mara wa jackpot, amesema pia alikuwa ameandaa mkeka wa kubashiri jackpot ya 16/16 iliyokuwa na zawadi ya zaidi ya fedha ya Kitanzania Sh800 milioni, lakini hakufanikiwa kuweka tiketi hiyo kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha wakati huo.
Akizungumzia mafanikio hayo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick, amesema washindi hao wawili wanaonyesha namna ambavyo sekta hiyo inabadilika na kukua.
“Kinachofanya hadithi hizi kuvutia si tu ukubwa wa ushindi wenyewe, bali pia watu waliopo nyuma ya ushindi huo. Grace na Husna wanatoka katika vizazi tofouti na kila mmoja ana simulizi yake ya maisha. Lakini wote wameunganishwa na jambo moja, ambalo ni kushuhudia ushindi uliobadilisha maisha yao kupitia majukwaa yetu. Hii ni uthibitisho kwamba fursa za mafanikio zinaweza kumpata mtu yeyote, bila kujali umri wake au maisha aliyopitia,” amesema.
Simulizi za Grace na Husna zinaakisi ukuaji wa ushiriki wa wanawake katika michezo nchini Tanzania, ambapo wengi zaidi wanaendelea kushiriki katika michezo ya kubahatisha kama Aviator na Supa Jackpot.
Kwa pamoja, simulizi zao zinatuma ujumbe mkubwa kwa Watanzania ambao ni wanawake sio tu wanashiriki katika burudani ya michezo hiyo ya kubahatisha, bali pia wanashinda ushindi mkubwa, wanavunja rekodi na kubadilisha mtazamo wa jamii katika kila hatua ya maisha.