Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wambura:TFF haiwezi kumng'oa Manji Yanga

Muktasari:

Michael Wambura amesema TFF ilitakiwa kuangalia mapungufu yaliyopo katika Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kisha kuiagiza Kamati ya Utendaji kuyafanyia kazi kisha watoe baraka za uchaguzi.

WAKATI leo Jumamosi Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likitaka kuingia katika zoezi la mchujo wa wagombea wa uchaguzi wa klabu ya Yanga aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Micheal Wambura ameibuka na kusema, Yusuf Manji bado ni bosi wa Yanga kwa baraka za shirikisho hilo.
Wambura ambaye kwasasa yuko nje akipambana mahakamani kupangua kifungo chake cha kufungiwa maisha kwa kuomba tafsiri ya kisheria, ameliambia Mwanaspoti kuwa kila anapowaona TFF wakimkataa Manji anajikuta anacheka kutokana na shirikisho hilo kuyumba.
Akitumia dakika 17:06 kuchambua hoja za TFF, Wambura alisema maamuzi ya Yanga kumkataa Manji yalipaswa kutokea Kamati ya Utendaji ya Yanga na Mkutano Mkuu wa wanachama au hata katiba ya klabu hiyo endapo ingebainisha.
Kigogo huyo mtata kwa masuala ya kisheria alisema TFF inapaswa kuiheshimu Yanga kutokana na klabu hiyo ni taasisi iliyosajiliwa kihalali na wana katiba yao ambayo inapaswa kuheshimiwa.
Alisema Manji baada ya kujiuzulu inajulikana wazi uamuzi wake haukukubaliwa na Wanachama, Baraza la Wadhamini lakini maamuzi pia ya Kamati ya Utendaji ambayo katiba yoyote ya Yanga na hata TFF inawatambua kwamba wana maamuzi ya mwisho nao waligomea uamuzi huo.
Aliongeza akisema juu ya yote TFF ilijichanganya kwa kumng'oa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Clement Sanga kisha kumtambua Manji kuwa ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo ambapo hata shirikisho hilo lilikuwa na baraka za kiongozi huyo kuwa mtu halali kuiongoza Yanga.
"Sijajua watu wanayumba wapi na Yanga kama watakubali hilo watakuwa wameharibu msimamo wa klabu yao,TFF haina mamlaka ya kumkataa Manji sasa unajua hili suala ni rahisi Yanga ni taasisi iliyosajiliwa na ina katiba yake.
"Tunatakiwa kuitumia katiba ya Yanga na kama katiba yao haisemi ndiyo tunatakiwa kuitumia katiba ya TFF lakini katiba zote hizo zinasisitiza maamuzi ya Kamati ya Utendaji ndiyo uamuzi wa mwisho.
"Yanga wenyewe wanasema Manji ni kiongozi wao na nimesikia kaandika barua kusema anarudi,ningekubaliana na TFF kama maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Yanga na Kamati ya Utendaji wangesema hawamtaki Manji hapo TFF ingekuwa na hoja.
"TFF inajichanganya tu na kuleta vurugu za maslahi yao watu wanatakiwa kujua TFF haohao ndiyo walibariki kusema Manji ni kiongozi halali wa Yanga kwahiyo Manji kuwa Mwenyekiti wa Yanga kuna baraka, wamesahahu walifanya maamuzi ya kumuondoa Sanga  kwa kuangalia maslahi yao?

KAMATI YA UCHAGUZI
Akigeukia upande wa uchaguzi wa Yanga kusimamiwa na TFF, Wambura alisema hata eneo hilo nalo lina mapungufu kama TFF ilichotakiwa kufanya hivyo endapo wangegundua katiba ya Yanga ina tatizo walipaswa kufika kwa msajili na kupata muongozo.
Wambura alisema TFF ilitakiwa kuangalia mapungufu yaliyopo katika Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kisha kuiagiza Kamati ya Utendaji kuyafanyia kazi kisha watoe baraka za uchaguzi.
"Walichotakiwa kufanya TFF ni kuitaka Kamati ya Utendaji ya Yanga kuyafanyia kazi mapungufu ya kamati yao ya uchaguzi kisha kuipa kazi ya kusimamia uchaguzi labda waniambie Yanga haina hata Kamati ya Utendaji."