Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WALETENI EVERTON

Muktasari:

Ikiongozwa na Kocha Msaidizi, Masudi Djuma kama Kaimu Kocha Mkuu, Simba iliibana Kakamega na kwenda nao kwenye matuta na kushinda penalti 5-4 na kutinga fainali ya michuano hiyo wakisaka tiketi ya kuifuata Everton nchini Uingereza mwezi ujao.

NI kweli Simba imecheza dakika 180 ya SportPesa Super Cup ikiwa na washambuliaji watano bila kufunga bao lolote, lakini ukweli ni kwamba jana imeutafuna mfupa ulioishinda Yanga ikiwang’oa Kakamega Homeboys ya Kenya kwa mikwaju ya penalti.

Ikiongozwa na Kocha Msaidizi, Masudi Djuma kama Kaimu Kocha Mkuu, Simba iliibana Kakamega na kwenda nao kwenye matuta na kushinda penalti 5-4 na kutinga fainali ya michuano hiyo wakisaka tiketi ya kuifuata Everton nchini Uingereza mwezi ujao.

Nahodha wa zamani na mchezaji mwendamizi wa Simba, Jonas Mkude kwa mara nyingine alikuwa shujaa kwa kufunga mkwaju wa mwisho wa timu yake na kuipeleka fainali na Jumapili itavaana na Gor Mahia iliyopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United katika mechi ya pili ya nusu fainali kwenye Uwanja wa Afraha, mabao yote yakifungwa na Meddie Kagere anadaiwa kuja Yanga.

Simba ilionyesha uhai tofauti na mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Kariobangi Sharks huku ikitengeneza nafasi na kushambulia lango la Wakenya, kiasi cha kuwaweka roho juu.

Adam Salamba, Marcel Kaheza, Mohammed Rashid, Moses Kitandu na Juma Rashid wakisaidiwa na Shiza Kichuya walishindwa kufunga mabao ndani ya dakika 90, licha ya kufanya kosa kosa nyingi ndani ya muda wote wa mchezo huo.

Mechi ya jana ni nne kwa Simba bila kupata ushindi ndani ya dakika 90 tangu ilipolala kwa Kagera Sugar siku wakikabidhiwa taji lao la Ligi Kuu Bara, kwani baada ya kipigo cha Wakata Miwa wa Kagera, Simba ilitoka sare ya 1-1 na Majimaji katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu kisha kutoka suluhu na Kariobangi na Kakamega za Kenya.

Katika mikwaju ya penalti ya jana Simba ilitupia zote tano kambani kupitia kwa Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Shiza Kichuya na Mkude aliyemaliza kazi, huku Kakamega iliyowafunga Yanga mabao 3-1 ikipoteza moja ya mwisho.

Lechantre asusa

Kabla ya mchezo huo wa jana mchana, Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre aliamua kususa kwa kujiweka kando yeye na Msaidizi wake, Mohammed Habib Aymen na kuiacha kazi kwa Djuma na Muharami Mohammed ‘Shilton’.

Lechantre na Habib walikaa jukwaani huku akifuatilia mchezo huo, ikielezwa imetokana na kumaliza mikataba yao na huku wakiwa hawaongezewi.

Mwanaspoti lililofichua kuwa, mkataba wa Mfaransa huo uliisha tangu Mei 29 na alifanya kikao na bilionea Mohammed Dewji ‘MO’ lakini hawakufikia makubaliano.

Ahadi ni kwamba mazungumzo yangeendelea baada ya michuano hiyo ya SportPesa na jana mwandishi wa Mwanaspoti aliyekuwepo Afraha, alimuuliza Mfaransa huyo kisa cha kukaa jukwaani na kufunguka.

“Nimempa nafasi Djuma aonyeshe uwezo wake kwani mkataba wangu umeshamazika na ninasubiri kufahamu hatma ya mkataba wangu mpya,” alisema Lechantre. “Rais wa Simba (Salim ‘Try Again’ Abdallah) hakuwepo katika mechi ya kwanza hapa na leo yupo uwanjani, nasubiri kujadiliana naye ili nijue nitabaki Simba ama la,” alisema.

Mabosi wa Simba licha ya kutoweka bayana, lakini inaelezwa wanaendesha msako wa kimya kimya wa kumleta Kocha Mkuu mpya kuchukua nafasi ya Lechantre ikielezwa gharama zake haziendani na soka inalocheza timu hiyo iliyobeba taji la Ligi Kuu 2017-18.