Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji wafafanua ushirikina

Muktasari:

Mwanaspoti lilipata nafasi ya kuzungumza na kipa wa Lipuli, aliona nini mpaka kuamua kwenda kuingilia kwenye kibendera!  Ally alijibu kama ifuatavyo "Kwenye mpira kuna vitu vizito, pengine kuliko unavyodhani kwa kutazama mpira unavyochezwa.

KILE kilichodaiwa ni ushirikina baina ya wachezaji wa Simba na Lipuli, katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa juzi Ijumaa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kimefafanuliwa na wachezaji ambao wamefanya tukio hilo waliodai mchezo huo una vitu vizito tofauti na wanavyotazamwa na mashabiki wao.
Alianza kiungo wa  Simba, Hassan Dilunga kugoma kutoka uwanjani baada ya kumalizika dakika 45 za mwanzo, alikuwa anamsubiri Ibrahim Job wa Lipuli atoke kwanza kisha yeye awe wa mwisho, kitu hicho kiliwastaajabisha mashabiki wengi.
Kipindi cha pili kipa wa Lipuli, Mohamed Ally na Miraji Athuman waliingia uwanjani kwenye kocha sehemu ya kibendera, vituko hivyo vilizidi kuleta tafsiri ya aina yake katika mechi hiyo, iliyoisha kwa suluhu.
Mwanaspotili lilipata nafasi ya kuzungumza na kipa wa Lipuli, aliona nini mpaka kuamua kwenda kuingilia kwenye kibendera!  Ally alijibu kama ifuatavyo "Kwenye mpira kuna vitu vizito, pengine kuliko unavyodhani kwa kutazama mpira unavyochezwa.
"Hizo ni imani za mtu husika unayemuona anafanya hivyo, ingawa mwisho wa picha soka ni uwanjani na dakika 90 lazima zitatoa mavuno kwa kila aliyecheza, mavuno yetu leo ni kuambulia pointi moja dhidi ya Simba,"alisema.
Kwa upande wa Athuman alitoa sababu ya kuingilia kwenye kibendera kuwa ilikuwa mbinu ya kuwatoa mchezoni wachezaji wa Simba kuhakikisha wanapunguza kasi ya mashambulizi.
"Unajua mpinzani anapoanza kukufanyia vituko, wewe fanya zaidi yake hapo ndipo unapommaliza mpinzani wako, nimeona mbinu zetu zimefanikiwa kupata suluhu ugenini na timu kama Simba si jambo dogo,"alisema.

SONSO, BOCCO MGUU KWA MGUU
Kama kuna tabu aliyoipata straika wa Simba, John Bocco kushindwa kuliona lango la Lipuli ni kibano cha beki Ally Mtoni alimaarufu kama Sonso ambaye hakumwachia hata nafasi ya kupumua.
Sonso alifichua kitu usichokijua kilichofanya ambane Bocco kuwa ni ubora wake  aliona angecheza naye mbali basi ndiye mchezaji pekee ambaye angeilaza mapema Lipuli.
"Bocco nilikuwa naye kwenye kambi ya timu ya Taifa Stars, nilimsoma vizuri kwenye mazoezi, kiukweli ni mchezaji anayejitambua na ndio maana muda wote nilimganda yeye nadhani hata alikuwa anashikwa na hasira, uzuri wa soka ukitoka uwanjani kila kitu kinakuwa kimeisha.
"Kuelekea michuano yao ya kimataifa, naamini Simba watafika mbali kwa sababu wana mastraika wazuri na makini Bocco , Meddie Kagera na Emmanuel Okwi wataibeba Simba, kushindwa kutufunga hakuna maana kwamba makali yao yamepungua,"alisema.