Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Lingalangala: Manji ndio Mwenyekiti wetu

Muktasari:

Thobias Lingalangala amekubali kwa moyo mmoja kuachia nafasi ya kaimu mwenywkiti wa klabu ya Yanga baada ya kuona bariua ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

ALIYEPITISHWA kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Thobias Lingalangala, amefunguka kwamba hakaimu tena nafasi hiyo baada ya mwenyekiti kurudi.
Akizungumza na Mwanaspoti baada ya mkutano wa  baraza la wadhamini kumalizika, alisema hakuna sababu ya yeye kuendelea kukaimu nafasi hiyo kwani katiba haimruhusu.
"Barua tayari imeshaandikwa na Mwenyekiti kwamba anarejea kwa hiyo mimi naqezaje kukaimu nafasi hii, nilikaimu kwa sababu mwenyekiti hakuwepo na si vinginevyo," alisema.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini, George Mkuchika, alisema nafasi ya Lingalangala haitambuliwi lakini hivi sasa hakuna tofauti baina yao na Lingalangala.
"Lingalangala hana tofauti yoyote hata na Lukumay wala sisi, tayari wameshashikana mikono na tupo nae pamoja sisi Yanga ni watu wa moja," alisema.