Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yang'ara FEÀSSA kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu

TANZA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika mkoani Morogoro kuanzia Agostii 12, 2026, Rais wa Shirikisho la FEASSA, Justus Mugisha amesema kwa upande wa shule za msingi mshindi wa jumla ni Kenya ikifuatiwa na Rwanda, na watatu Tanzania huku kwa shule za sekondari wa kwanza Kenya, wa pili Uganda na wa tatu Tanzania.

Mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSA) 2026, yamemalizika ambapo Tanzania imeendelea kushika nafasi ya kwanza mara ya tatu mfululizo kwenye michezo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika mkoani Morogoro kuanzia Agostii 12, 2026, Rais wa Shirikisho la FEASSA, Justus Mugisha amesema kwa upande wa shule za msingi mshindi wa jumla ni Kenya ikifuatiwa na Rwanda, na watatu Tanzania huku kwa shule za sekondari wa kwanza Kenya, wa pili Uganda na wa tatu Tanzania.

Ameeleza kuwa, mashindano hayo yamekuwa na tija hasa katika kuibua vipaji vya wanamichezo ambapo baadhi yao huwa wanapata fursa ya kuingia katika soko la ushindani katika ligi mbalimbali.

TAN 01

Amesema kufanyika kwa mashindano hayo mkoani Morogoro, kunatoa fursa ya kuanza safari mpya ya mashindano yanayofuata mwaka 2027 yatakayofanyika Kigali nchini Rwanda ambapo pia yatafanyika maboresho ikiwemo matumizi ya teknojia.

"Tushukuru mashindano kufanyika Morogoro, imekuwa fahari kwetu yamemalizika salama tukijivunia ukarimu na mazingira ya kuvutia kwa washiriki wote, baada ya hapa sasa ni zamu ya Kigali, tunaamini tutafanya vizuri zaidi na maboresho yatakuwa makubwa sana ikiwemo teknolojia na kuongeza idadi ya washiriki," amesema Mugisha.

TAN 02

Akifunga mashindano hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Festo Dugange, amewataka washiriki kutumia michezo hiyo  kujenga na kuimarisha ushirikiano, umoja na amani.

Naibu Waziri huyo amebainisha kuwa michezo hiyo sio tu kwaajili ya kuimarisha afya za wachezaji bali inadumisha amani, upendo na kuimarisha mshimamano kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema pamoja na kuimarisha mshikamano, pia michezo hiyo imekuwa fursa kwa wanafunzi kujifunza tamaduni za mataifa ya afrika Mashariki ambapo yatasaidia katika kujenga undugu na kuondoa matabaka yanayoweza kujitokeza kutokana na changamoto za kisiasa.

TAN 04

"Niwapongeze sana waandaji wa mashindano haya kwa vijana wetu wa shule za msingi na sekondari kwa sababu uwepo wa mashindano haya imekuwa fursa kwako kujifunza tamaduuni za mataifa yetu lakini pia kuwawezesha kudumisha amani upendo na mshikamano uliopo katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki," amesema Dugange.

Dugange amewataka waandaaji wa mashindano kuboreshwa zaidi  kwa kutumia teknolonia ya habari ili kutunza vizuri kumbukumbu za michezo hiyo ikiwemo na kuonesha marejeo ya matukio wakati michezo ikiendelea.

Mashindano ya FEASSA  mwaka 2026 yamehusisha michezo mbalimbali na kushirikisha wanafunzi, makocha na walimu zaidi ya 6000 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.