Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania U-15 yang’ara Azerbaijan

TANZANIA Pict

Muktasari:

  • Pia kulikuwa na mabadiliko ya hali ya hewa kidogo; leo kulikuwa na baridi sana na mvua mvua kidogo, lakini vijana wameweza kuzoea hali hiyo na wamecheza vizuri, amesema kocha huyo.

KOCHA wa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 15 (U-15), Mohamed Amin amesema vijana wake wameanza kuzoea mazingira ya mashindano ya World Cup Festival yanayoendelea Baku, Azerbaijan, jambo lililowasaidia kufanya vizuri na kupata ushindi katika mechi mbili walizocheza.

Amin amesema hayo baada ya timu hiyo kucheza mechi tatu ikishinda mechi mbili na kupoteza moja dhidi ya Uruguay 1-0, na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Comoro kabla ya kuichapa Montserrat kwa mabao 6-1, matokeo yanayoonyesha namna vijana hao walivyozidi kuimarika.

Ukiangalia hapo kuna mabadiliko kwa vijana; wameanza kuzoea na leo kidogo wameweza kutoa ule uoga na kucheza ule mchezo wao,  amesema Amin.

TANZA 01

Kocha huyo amesema mwanzoni vijana walikuwa bado wanajifunza kuendana na mazingira mapya ya mashindano hayo, lakini kadri muda unavyokwenda wamekuwa wakipata ujasiri na kuonyesha kile wanachoweza kufanya, jambo analoliona kuwa ishara nzuri kwa timu hiyo.

Amin pia alizungumzia changamoto ya hali ya hewa, akisema baridi kali na mvua za hapa na pale vilikuwa miongoni mwa mambo ambayo vijana walilazimika kuyakabili, lakini waliweza kuzoea hali hiyo na kucheza vizuri katika mechi hizo mbili.

TANZA 02

Pia kulikuwa na mabadiliko ya hali ya hewa kidogo; leo kulikuwa na baridi sana na mvua mvua kidogo, lakini vijana wameweza kuzoea hali hiyo na wamecheza vizuri, amesema kocha huyo.

Akizungumzia michezo inayofuata, Amin amesema Tanzania inatarajia kukutana na Moldova na Uruguay, huku akitoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwaunga mkono vijana hao wanaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo.