Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba walivyotua Misri kitajiri, Al Ahly waingiwa ubariidiii!

AL Ahly wameingiwa ubaridi kutokana na kishindo cha Simba ilichotua nacho Jijini Cairo juzi.

Simba wametua kitajiri na kufikia kwenye hoteli ya maana huku wakiwa hawana presha yoyote kama ilivyokuwa miaka ya nyuma walivyokuwa wakiingia Misri kwa presha ya kula vipigo vikubwa.

Simba haina cha kupoteza wakati itakapokabiliana na Ahly kesho Ijumaa jambo ambalo limeonekana kutowafurahisha mashabiki wa Waarabu hao.

Kitendo cha Simba kuongoza kundi A hata ikipoteza mechi hiyo, kimetajwa kuwa pigo na Al Ahly ambayo imedai kuwa mpango wao ulikuwa kumaliza ikiwa kinara wa kundi A ili iwakwepe Mamelodi Sundowns walio tishio katika mashindano hayo

Nyota wa zamani wa Al Ahly, Walid Salah El-Din amedai ingekuwa jambo jema kwa Al Ahly kuongoza kundi lake, lakini bahati mbaya kwao Simba imevuruga hilo na sasa ndio yenye faida ya kukutana na vibonde watakaomaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi yao. Eldin alisema takwimu zisizovutia za Al Ahly ugenini zinampa wasiwasi huenda wakawa katika wakati mgumu kwenye hatua inayofuata kutokana na ubora wa timu watakazokutana nazo. “Kizazi cha sasa cha Al Ahly sio hatari ugenini kulinganisha na kile chetu cha Mohamed Barakat na Emad Meteb. Walikuwa na bahati ya kucheza katika Kombe la Dunia la Klabu kule Qatar katika mazingira yanayofanana na ya Misri, lakini matokeo yangekuwa tofauti kama wangechezea Japan.

“Natumaini Al Ahly itapangwa na timu kutoka Kaskazini mwa Afrika robo fainali na kuwakwepa Mamelodi Sundowns, hivyo hawatokuwa na ugumu kutetea taji,” alisema El-Din alipohojiwa na mtandao wa Kingfut wa Misri. Ikumbukwe mwaka 2019, Al Ahly ilikutana na Mamelodi Sundowns katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa kwa mabao 5-1 ambapo ilifungwa 5-0 ugenini Afrika Kusini na kushinda 1-0 nyumbani.


LUIS AWAKIMBIZA

Katika hatua nyingine, Luis Miquissone amewaacha kwenye mataa nyota wa Al Ahly akiteuliwa mara nyingi katika kikosi bora cha wiki cha hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, jambo ambalo halijafanywa na mchezaji yeyote wa Al Ahly hadi sasa.

Kitendo cha kuteuliwa kikosi bora cha wiki cha raundi ya tano kimefanya iwe mara ya tatu kwake kulinganisha na nyota wa Al Ahly ambao baadhi wamechaguliwa mara mbili. Luis alichaguliwa kikosi cha wiki ya pili, akateuliwa ha wiki ya nne na juzi. Kiujumla, anashika nafasi ya pili na kinara wa kuteuliwa kikosi bora cha wiki cha makundi ya mashindano hayo kinachotangazwa na CAF ni beki wa kati wa MC Alger, Mouad Ellafi aliyechaguliwa mara nne. Wanaomfuatia Luis ni Mohamed Magdi Afsha na Mohamed Hany wa Al Ahly ambao kila mmoja kateuliwa mara mbili sawa na Mosa Lebusa (Mamelodi) na Ayoub El Kaabi wa Wydad Casablanca.