Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Day 2026 kufanyika Uwanja wa Uhuru Agosti 8

WAWI 03
WAWI 03

Muktasari:

  • Ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa la kipekee kwa kuwa litakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 90 ya Simba Sports Club, huku mashabiki wakitarajiwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuadhimisha historia ya klabu hiyo.

Klabu ya Simba imetangaza kuwa kilele cha tamasha la Simba Day 2026 kitafanyika Agosti 8, 2026 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku kikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema hayo leo Jumatano Julai 22, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema awali walikuwa na matarajio ya kufanyia tamasha hilo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na ukubwa wa tukio hilo, lakini uwanja huo upo kwenye matengenezo.

“Simba Day 2026 itafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru. Kutokana na ukubwa wa tamasha hili duniani tunatamani kufanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, lakini kwa sasa upo kwenye matengenezo hivyo uwanja ambao utatumika ni Uwanja wa Uhuru,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa la kipekee kwa kuwa litakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 90 ya Simba Sports Club, huku mashabiki wakitarajiwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuadhimisha historia ya klabu hiyo.