Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saa 48 za maajabu Yanga

Dar es Salaam.  Kaimu Katibu Mkuu mpya wa Yanga, Omari Kaaya ametangaza kufanya maajabu ndani ya saa 48 zijazo kwa kuirejesha klabu hiyo katika hali ya utulivu.
Kauli ya Kaaya imekuja kutokana na Yanga kulazimika kufanya usajili wa wachezaji wake ndani  saa 48 kabla ya kufungwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kaaya alitangazwa jana kujaza nafasi ya Charles Mkwasa, aliyetangaza kujiuzulu wadhifa wake kwa sababu za afya. Mbali na Mkwasa, Yanga pia ilimpoteza Makamu Mwenyekiti wake Clement  Sanga, aliyejiuzulu kwa madai ya kutishiwa kuuawa.
Sanga anaungana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga kujiuzulu akitanguliwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Ayoub Nyenzi, Hashimu Abdallah, Salum Mkemi na Omari Saidi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alimtangaza Kaaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu baada ya kudumu katika wadhifa wa ofisa masoko ndani ya klabu hiyo.
Ten alisema Wajumbe wa Baraza la Wadhamini walipitisha jina la Kaaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga.
Kaaya alisema jukumu lake la kwanza baada ya kupewa kazi hiyo ni kuhakikisha ndani ya saa 48 zijazo, wachezaji wote watakuwa wametia saini mikataba ya kuitumikia Yanga msimu ujao.
Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika ni Kelvin Yondani, Hassani Kessy, Juma Abdul, Benno Kakolanya na Geofrey Mwashiuya.
Pia alisema atahakikisha Yanga inacheza kwa kiwango bora mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Jumapili wiki hii.
Yanga inatakiwa kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kusonga mbele baada ya kulala mabao 4-0 ugenini kwenye Uwanja wa Kasarani, Kenya.
“Nimekubali kuvaa viatu vya Mkwasa (Charles), nina jukumu zito sana hasa hili la usajili, kuna baadhi ya wachezaji mikataba yao imemalizika na tunawahitaji watie saini tena. “Wachezaji wengine wapya wanatakiwa kusajiliwa, ni kipindi kigumu lakini nitajitahidi kupitia kamati zilizopo na wadau wengine kukamilisha zoezi hili gumu,” alisema Kaaya.
Yanga imekumbwa na mtikisiko wa kiuchumi tangu alipojiweka kando  Manji.
Klabu hiyo inapitia kipindi kigumu, baada ya kuyumba kiuchumi  hatua iliyochangia  kufanya usajili wa kusuasua licha ya kubakiwa na saa 48 kabla ya dirisha kufungwa kesho saa sita usiku.
Yanga ilipata Sh900 milioni zinazotolewa kwa awamu kwa mwaka zikiwa ni fedha za wadhamini SportPesa.
Wakati Kaaya akijinasibu kuivusha Yanga, akaunti ya klabu hiyo imebakiwa na Sh2.1 milioni fedha ambazo ni mgawo wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Yanga ilipewa Dola 137,390 (Sh312 milioni), baada ya kufuzu hatua ya makundi ikiungana na timu za Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sport (Rwanda) na USM Alger ya Algeria.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini fedha hizo ziliingia katika akaunti ya Yanga Mei 15 na mara moja zilianza kutumika kulipia gharama mbalimbali yakiwemo madeni.
Taarifa ya fedha ambayo gazeti hili inayo inaonyesha Yanga ilitumia Sh140.2 milioni kulipa madeni ya wachezaj  Februari na Machi, mishahara ya waajiriwa miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba Sh40.3 milioni.
Yanga ilimlipa Sh20 milioni mmoja wa mwanachama wake (jina tunalo) ikiwa rejesho (mkopo) wa fedha alizoikopesha, Sh60.5 milioni zilitumika kulipa mishahara ya benchi la ufundi Januari na Februari.
Pia Sh11.7 milioni ikiwa ni malipo ya tiketi za maofisa wa mechi  waliochezesha mechi dhidi ya Rayon Sport, Sh6 milioni kulipia gharama ya kambi ya Yanga.Sh11.4 milioni zilitumika kulipia moja ya malipo ya usajili Sh3.6 milioni kulipia kambi ya mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar, Sh5. milioni kulipa bonansi kwa wachezaji.
Fedha hizo pia zilitumika kulipia kambi ambazo ni Sh4.1 milioni ilipokuwa ikijiandaa na mechi dhidi ya Rayon Sports.