Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prison, Coastal Union shoo ya kibabe

Muktasari:

  • Tanzania Prison na Coastal zimeshindwa kutambiana baada ya kutoshana sare ya kufungana magoli 2_2 katika uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Timu ya Tanzania Prison imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 2-2 dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.

katika mchezo huo uliokuwa wa kasi na kuvutia kwa timu zote mbili ulishuhudia wenyeji Prison wakijiandikia bao la kuongoza kunako dakika ya 19, ya mchezo kupitia kwa Samson Mbangula kumtoka kipa wa Coastal, Abubakar Abas baada ya mabeki wa Coastal Union kudhani mchezaji huyo ameotea.

Licha ya kutanguliwa bao hilo ila Coastal ilirejea mchezoni na kusawazisha bao hilo kunako dakika ya 23 kupitia kwa Abdul Hamis kwa mkwaju wa penati baada ya Marco Mhilu kunawa mpira katika eneo la hatari.

Prison ilijibu mashambulizi ya Coastal kwa kujipatia bao la pili kunako dakika ya 35 ya mchezo kupitia kwa Jeremia Juma baada ya shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Coastal Union, Abubakar Abas.

Hata hivyo Coastal haikukata tamaa kwani ilibidi kusubri mpaka dakika za lala salama kwa kusawazisha bao hilo dakika ya 85 ya mchezo kupitia kwa Mudathir Abdallah aliyeingina kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Raizin Khafidhi aliyeonekana kukosa nafasi za wazi kunako kipindi cha kwanza cha mchezo.

Kwa matokeo haya Tanzania Prison inashika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 42 katika michezo 32. huku ikisaliwa na michezo miwili ambayo ni dhidi ya Kagera Sugar na Gwambina.

Matokeo hayo yanakuwa sio mazuri kwa Coastal Union katika janga la kujinasua kushuka daraja kwani inasalia katika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 34 katika michezo 31 huku ikisaliwa na michezo mitatu ambayo ni dhidi ya Simba, Mwadui FC na Kagera Sugar.


IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI