Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Niyonzima aibukia katika uingiza Bongo Movie

Muktasari:

Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Myarwanda Haruna Niyonzima, ameingia rasmi kwenye burudani ya filamu.

Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregs' mbali na soka, ameibukia katika filamu moja ya Kiswahili inayoitwa The ring.

Niyonzima kwa sasa anacheza katika Klabu ya AS Kigali ya Rwanda baada ya kuachana na Simba.

Niyonzima amesema filamu hiyo itakuwa sokoni si muda mrefu ambapo yeye ametambulika kwa jila la Daniel na amechezwa na mwanamke mmoja maarufu kwa jina la Marry Blizzy.

Filamu hiyo inayohusu mapenzi na usaliti, imeongozwa na Valle Matambi na kuhaririwa na Said Mrisho na imechezwa na wasanii wengine kutoka Tanzania na Rwanda.

Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji wa soka kucheza filamu kwani awali, kocha wa zamani wa Simba na Taifa Stara, Mbrazil Marcio Maximo aliwahi kuigiza katika moja ya filamu.

Kitendo hicho kinamfanya, Niyonzima baada ya kuwapa raha wapenzi wa soka wa klabu mbili za Simba na Yanga, sasa ni zamu ya mashabiki wa filamu.