Ninja, Zahera wana siri nzito
Muktasari:
- Kuhusu Cannavaro alisema;”Ni kaka yangu ananifuatilia hatua moja hadi nyingine, jambo kubwa nikikosea ananiambia nikicheza vizuri ananitia nguvu huku akinishauri kusaka kucheza nje ya nchi.”
BEKI Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amefichua mafanikio yote aliyonayo yamechangiwa za Kocha Mwinyi Zahera na nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ninja alisema mafanikio makubwa aliyoyapata Yanga kwa muda mfupi yamechangiwa na Zahera aliyemtaja kama mmoja ya makocha bora kukutana nao, lakini akimtaka Cannavaro kwa kuchangia kusajiliwa kwake Jangwani.
“Mpaka hapa nilipofika ni kazi kubwa ya Zahera anayeniambia vitu vingi vya kiufundi akitaka niwe na nidhamu ya hali ya juu kwa maana ya kuheshimu muda wa mazoezi, kula na kupumzika,” alisema.
Kuhusu Cannavaro alisema;”Ni kaka yangu ananifuatilia hatua moja hadi nyingine, jambo kubwa nikikosea ananiambia nikicheza vizuri ananitia nguvu huku akinishauri kusaka kucheza nje ya nchi.”