Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nini kinafuata kwa Gerald Mathias Mdamu?

MSHAMBULIAJI mahiri wa klabu ya Polisi Tanzania, Gerald Mathias Mdamu amevunjika miguu yake miwili baada ya kupata ajali ya gari wakati timu hiyo ikitoka mazoezini mapema wiki iliyopita. Inasikitisha kwa mchezaji kama yeye anayeishi kwa kutegemea miguu.

Kazi yake ipo miguu mwake. Ajali kama hizi zinasikitisha zaidi zikitokea kwa mchezaji anayeishi bara hili na hasa nchi hii. Maelfu ya vijana wa dunia ya tatu ndoto zao za kucheza soka zimekwama baada ya kupata majeraha kama haya ndani na nje ya uwanja.

Matibabu ya mtu aliyevunjika miguu miwili Tanzania yana umakini gani? anatibiwa kwa ajili ya kucheza mpira au anatibiwa kwa ajili ya kurudi atembee kama kawaida? Nadhani kwa huku kinachotokea ni hili la pili. Hilo la kwanza sina uhakika nalo sana.

Wenzetu walioendelea viwango vya matibabu vipo juu zaidi. mchezaji anavunjika vibaya lakini wanamtibu ili aweze kurudi kucheza tena soka. Eduardo da Silva wa Arsenal ni miongoni mwa wachezaji ambao walivunjika vibaya kiasi kwamba tuliamini asingeweza hata kutembea tena lakini Wazungu wakamtibu ili acheze.

Sijui kama tutaweza kumtibu Mdamu ili acheze tena au tutamtibu kwa ajili ya kuhakikisha anatembea kama kawaida. Na kwa lolote lililomtokea tunaweza kujiuliza, je mchezaji mwenyewe alikuwa na bima?

Kuna bima za aina mbili. Kuna bima ya matibabu lakini pia kuna bima ambazo wenzetu huwa wanawekewa kama maisha yao ya soka yatakomea hapo. Sijui kama haya yote mawili yapo. Kama hayapo nadhani inabidi tujifunze kupitia hili.

Vinginevyo kilichomtokea Mdamu kinasikitisha sana na hasa kama ndoto zake za kucheza soka zitakomea hapo. Kama ndoto zake za kucheza soka zitakomea hapo basi walio karibu wanaweza kumtengenezea ndoto nyingine katika maisha.