Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nduwumwe atuma ujumbe Singida BS

Muktasari:

  • Nduwumwe anayecheza MC Algiers aliyojiunga nayo Agosti 7, 2026 akitokea Singida Black Stars, alisema katika kikosi hicho, anaamini wazawa waliopo wakicheza vizuri itakuwa mwanzo wa wao kuonekana na timu nyingine nje ya Tanzania

WAKATI Singida Black Stars ikijiandaa kwenda kucheza dhidi ya AS Maniema Union ya DR Congo, Novemba 28, 2026 katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Mossi Nduwumwe amewapa ushauri wachezaji wazawa kutumia vizuri fursa hiyo.

Nduwumwe anayecheza MC Algiers aliyojiunga nayo Agosti 7, 2026 akitokea Singida Black Stars, alisema katika kikosi hicho, anaamini wazawa waliopo wakicheza vizuri itakuwa mwanzo wa wao kuonekana na timu nyingine nje ya Tanzania.

“Wachezaji wa kimataifa ambao wanacheza Tanzania, wengi wao walionekana kupitia mechi kama hizo za CAF, hivyo wazawa wawe na wivu wa kutumia fursa hiyo na wao kwenda kupambana nje ya mipaka yao,” alisema Nduwumwe ambaye msimu wa 2025-2026 alimaliza kinara wa mabao Ligi Kuu Bara akifunga 17.

Alisema soka ni kazi yao, wakati mwingine mchezaji analazimika kuishi nje ya nchi alikozaliwa, ili kuhakikisha anatafuta kipato cha kuja kumsaidia kuishi vizuri baada ya kustaafu.

“Changamoto za kuishi nje na nyumbani zipo, lakini lazima kupambana nazo, hivyo wachezaji wa Tanzania wajitahidi kuona fursa kupitia michuano ya CAF watafika mbali, siyo Singida tu, kuna Azam, Simba na Yanga, zina wachezaji wenye viwango vya juu,” alisema na kuongeza;

“Kucheza nje kunaongeza thamani kwa mchezaji, mfano kuna Watanzania ambao majina yao yanatajwa mara kwa mara kutokana na walichokifanya kama Mbwana Samatta, hilo linawezekana kwa mchezaji yeyote anapoamua kupambana.”