Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndumbaro, Rage waingia uchaguzi Simba

Muktasari:

  • Simba ilitangaza kufanya uchaguzi Novemba 3, lakini wadau mbalimbali akiwemo mwanasheria mwenye uzoefu wa kutosha na masuala ya soka.

Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden

Rage amesema, kipengele cha elimu kwa mgombea wa nafasi ya urais

ndani ya klabu ya Wekundu hao wa Msimbazi kuwa na shahada

kinatakiwa kutupiwa jicho.

Rage amesema, pamoja na kanuni ya elimu, lakini watu wakumbuke

wazee walioongoza Simba hawakuwa na elimu ya digrii, lakini ndio

hao wameondoka na kuacha kumbukumbu ya majengo.

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania

(FAT) sasa TFF, amekwenda mbali na kusema kipengele hicho

kinaacha maswali kwa kuwa hakijafafanua shahada ipi inayotakiwa

kwa nafasi ya urais.

“Kipengele cha elimu hakijabainisha ni digrii ya nini inahitajika kwa

kuwa wapo watu wana digrii ya dini na wengine ya ushonaji.

"Kuhusu bei ya fomu kuwa  500,000 siwezi kuizungumzia, lakini cha

msingi nishauri wanachama wetu wa Simba wasome katiba na

kuilewa," alisema Rage.

Kwa upande wa Dk Damas Ndumbaro amesema,  Simba inapaswa

kufuata kanuni za uchaguzi za TFF  ili kuepuka mkanganyiko

unaoweza kuibua sintofahamu baina ya pande hizo mbili.

Ndumbaro alisema Simba ni mwanachama wa TFF na haina kanuni

za uchaguzi, hivyo inapaswa kufuata kikamilifu kanuni za uchaguzi za

Shirikisho hilo ili kupata viongozi halali.

"Kamati ya Uchaguzi ya Simba inapaswa kuheshimu kanuni za

uchaguzi za TFF, inawezekana kamati ya uchaguzi ya sasa labda

haina uzoefu lakini wanapaswa kusoma vizuri kanuni kuzielewa na

kuzifuata.

"Ingekuwa Simba ina kanuni zake ambazo zingepitishwa na TFF hilo

lingekuwa jambo jingine, lakini kwa sababu haina inatakiwa kutii kile

kilichoandikwa kwenye kanuni za uchaguzi za TFF,"alisema Dk

Ndumbaro.

Amesema, Simba inatakiwa kufuata kanuni kuhusu kiwango cha

elimu na gharama za ununuzi wa fomu ya uchaguzi kama ulivyoanishwa

na TFF.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba Boniphace Lyamwike

alidai kuwa hajapata taarifa rasmi za kusimamishwa uchaguzi huo.

"Hatujapata taarifa rasmi kwa sababu hakuna mawasiliano

yaliyofanyika kati ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kamati ya

Uchaguzi ya Simba.

Hata hivyo, Lyamwike alisema wanaendelea na mchakato wa

uchaguzi hadi watakapopata taarifa rasmi kuhusu kusimamishwa

uchaguzi.

"Hakuna tofauti kubwa Katiba ya Simba inaelekeza kama kutakuwa

hakuna kanuni za uchaguzi za Simba tutatumia za TFF.

“Kimsingi hakuna kanuni za uchaguzi Simba moja kwa moja, katiba

yetu imetuelekeza kwenda kwenye kanuni za TFF na tumefuata

kanuni za uchaguzi za TFF zinavyosema ikiwemo viwango walivyotoa

na ndio sisi tulivyopanga,” alisema mwenyekiti huyo.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF  Wakili

Revocatus Kuuli alisema uchaguzi wa klabu hiyo umesimamishwa kwa

kukiuka baadhi ya kanuni za uchaguzi.

"Wamepanga ada kuwa Sh500,000 na sifa za mgombea wa nafasi ya

mwenyekiti digrii, lakini kwa mujibu wa kanuni wanatakiwa kutumia

kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ambazo zinataka

mgombea awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na gharama za

kuchukua fomu kwa nafasi ya mwenyekiti Sh 200,000 na nafasi

nyingine Sh100,000,"alisema Kuuli.

Muda mfupi baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),

kusimamisha uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba, wadau wa michezo

wametoa maoni tofauti kuhusu hatima ya kinyang’anyiro hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Revocatus Kuuli,

alisema uchaguzi huo umesimamishwa kwa madai ya klabu hiyo

kukiuka baadhi ya kanuni ndani ya katiba.